Araqchi: Tunataka kukomeshwa vita kabisa, sio kusitishwa kwa muda
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137494-araqchi_tunataka_kukomeshwa_vita_kabisa_sio_kusitishwa_kwa_muda
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Tehran haikubali suala la kusitishwa mapigano, bali inataka kukomeshwa kabisa, kikamilifu na daima kwa vita hivyo.
(last modified 2026-03-21T06:33:22+00:00 )
Mar 21, 2026 06:33 UTC
  • Sayyid Abbas Araqchi
    Sayyid Abbas Araqchi

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Tehran haikubali suala la kusitishwa mapigano, bali inataka kukomeshwa kabisa, kikamilifu na daima kwa vita hivyo.

Sayyid Abbas Araqchi ambaye alikuwa akizungumza na shirika la habari la Kyodo la Japan amesema, nchi kadhaa zinafanya juhudi za upatanishi kwa ajili ya kukomeshwa vita na Iran inakaribisha ubunifu wowote unaolenga kukomeshwa kabisa, kikamilifu na daima kwa vita vya sasa.

Araqchi amesema: Hatujafunga Lango Bahari la Hormuz lakini tumeweka masharti na vizingiti kwa meli za nchi zinazoshiriki katika mashambulizi dhidi ya nchi yetu.

Waziri  wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Tehran imeanza mazungumzo na Japan juu ya uwezekano wa kufunguliwa Lango Bahari la Hormuz na kwamba Iran iko tayari kuziruhusu meli za Japan kupita katika lango bahari hilo.

Sayyid Abbas Araqchi amesema hadi sasa Marekani haijaonyesha utayarifu unaohitajika kwa ajii ya kufikia suluhisho haisi.