Mokhber: Taifa lenye irada na azma ya atomiki halihitaji bomu la atomiki
-
Mohammad Mokhber
Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe kwenye mitandao ya kijamii akisema: Taifa lenye irada na azma ya atomiki halihitaji bomu la atomiki.
Katika ujumbe huo uliochapishwa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, Mohammad Mokhber amesema: Taifa lenye idara na azma ya atomiki halihitaji bomu la atomiki.
Ameongeza kuwa: Miongoni mwa matokeo ya ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu katika vita vya kutwishwa vya sasa na kuainishwa mfumo mpya kwa ajili ya Lango Bahari la Hormoz ni kudhoofika Petrodola na kuanza mchakato wa kuangamia Mr Dollar, kuongezeka mahitaji ya riyali ya Iran, kupatikana kipato cha kuaminika kwa Iran, na Jamhuri ya Kiislamu kubadilika kutoka nchi iliyowekewa vikwazo na kuwa taifa linaloweka vikwazo.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kwamba itaweka utaratibu mpya wa usafirishaji wa meli kupitia Lango Bahari la Hormuz na kwamba haitaruhusu maadui wake kutumia njia hiyo ya kimkakati ya majini.