The Independent: Trump analazimika kuipa Iran inachokitaka ili kujinasua kwenye maangamizi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137506-the_independent_trump_analazimika_kuipa_iran_inachokitaka_ili_kujinasua_kwenye_maangamizi
Gazeti la Uingereza la Independent limeandika kuwa, Rais Donald Trump wa Marekani amenasa katika maangamizi kwa kuanzisha vita dhidi ya Iran na analazimika kuipatia Iran inachokitaka ili kukomesha vita hivyo.
(last modified 2026-03-22T04:06:13+00:00 )
Mar 22, 2026 03:49 UTC
  • The Independent: Trump analazimika kuipa Iran inachokitaka ili kujinasua kwenye maangamizi

Gazeti la Uingereza la Independent limeandika kuwa, Rais Donald Trump wa Marekani amenasa katika maangamizi kwa kuanzisha vita dhidi ya Iran na analazimika kuipatia Iran inachokitaka ili kukomesha vita hivyo.

Ripoti ya gazeti hilo la Uingereza imefichua kwamba kutokana na kuendelea mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran, Rais wa Marekani amejitumbukiza katika vita ambavyo hana uwezo wa kujinasua na mashaka yake.

Uchambuzi wa gazeti hilo la Uingereza unaendelea kusema: Donald Trump hawezi tena kudai kwamba anashinda vita, kwa sababu Iran inaendelea kutoa vipigo; hivyo Trump analazimika kuwapatia Wairani wanachokitaka.

Independent limeongeza kuwa, operesheni za Marekani zinafanyika kwa mwendo wa kinyonga zikiendelea kulimomonyoa na kulichosha jeshi la nchi hiyo, na Trump anashuhudia kwa macho machaguo yake yakiyoyoma. “Sasa amekuwa kichekesho kwa kadiri kwamba amekuwa tegemezi kwa irada na maamuzi ya Wairani kwa ajili ya kujiondoa kwenye vita, na anahitaji kuona Iran ikisimamisha mashambulizi dhidi ya Israel; na muhimu zaidi ifungue Lango Bahari la Hormuz kwa usafirishaji wa meli,” limeandika gazeti la Independent.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa: Karibuni, Trump atalazimika kuwaomba Wairani kwa heshima waondoe buti lao kwenye koo la uchumi wa Magharibi, na badala yake, wao pia wapewe wanachokitaka.

Gazeti hilo linaandika: Kwa msingi huo mashambulizi ya mabomu na mauaji ya kigaidi kwa ajili ya kuiangusha Jamhuri ya Kiislamu hayakuwa na faida yoyote. Sasa umewadia wakati wa Trump kufanya muamala na Iran na kujinasua kwenye maangamizi.