Iran yatoa onyo kuhusu hujuma dhidi miundombinu ya nishati na mafuta
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137510-iran_yatoa_onyo_kuhusu_hujuma_dhidi_miundombinu_ya_nishati_na_mafuta
Msemaji wa Kamandi ya Jeshi la Iran ya Khatam al-Anbiyaa (SAW) ametoa onyo kali kuhusu uwezekano wa kushambuliwa kijeshi miundombinu ya nishati na mafuta ya Iran.
(last modified 2026-03-22T05:03:35+00:00 )
Mar 22, 2026 05:03 UTC
  • Ibrahim Zolghadari,
    Ibrahim Zolghadari,

Msemaji wa Kamandi ya Jeshi la Iran ya Khatam al-Anbiyaa (SAW) ametoa onyo kali kuhusu uwezekano wa kushambuliwa kijeshi miundombinu ya nishati na mafuta ya Iran.

Kulingana na ripoti kutoka Shirika la Habari la Tasnim, Ibrahim Zolghadari, msemaji wa kituo hicho, amesema: “Kufuatia onyo za awali, ikiwa miundombinu ya mafuta na nishati ya Iran itashambuliwa na adui, basi, miundombinu yote ya nishati, teknolojia ya habari, na mitambo ya kusafisha maji inayomilikiwa na Marekani na utawala wa Kizayuni katika eneo hili itakuwa lengo la mashambulizi.”

Shirika la Habari la Tasnim limeripoti kwamba mtawala wa Marekani Donald Trump ametishia kupitia mitandao ya kijamii kwamba iwapo Iran haitafungua Lango Bahari la Hormuz kwa meli zote, basi Marekani itashambulia miundombinu ya nishati ya Iran. Trump ametishia wazi kwamba ataanza kwa kushambulia kituo kikubwa zaidi cha kuzalisha nishati cha Iran. Baada ya Trump kushindwa kutumia jeshi la Marekani kusindikiza meli za mafuta sasa anatoa vitisho vya kushambulia miundombinu ya nishati ya Iran ili kuilazimu Tehran iruhusu meli zote zipite katika njia hiyo muhimu ya bahari.

Iran imesisitiza kuwa itatekeleza sera ya jicho kwa jicho katika kujibu jinai za Israel. Katika fremu hiyo, juzi baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kutekeleza hujuma dhidi ya kituo cha nyuklia cha Natanz nchini Iran,  Jeshi la Iran limejibu kwa kutekeleza shambulio dhidi ya kituo cha nyuklia za Dimona cha utawala wa Israel na kusababisha hasara kubwa.

Aidha hivi karibuni pia , baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kushambulia kiwanda kikubwa cha gesi cha Pars Kusini nchini Iran, Jeshi la Iran limejibu kwa kushambulia kwa mafanikio makubwa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Haifa.