Iran yazitahadharisha nchi zinazotumia ugaidi kujinufaisha
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i16798-iran_yazitahadharisha_nchi_zinazotumia_ugaidi_kujinufaisha
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezitahadharisha nchi zinazotumia ugaidi kufikia malengo na maslahi yao ya kibinafsi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 05, 2016 11:21 UTC
  • Iran yazitahadharisha nchi zinazotumia ugaidi kujinufaisha

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezitahadharisha nchi zinazotumia ugaidi kufikia malengo na maslahi yao ya kibinafsi.

Hayo yamesema na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya nchi za Kiarabu na Kiafrika hapa mjiniTehran katika mazungumzo na Sigrid Kaag, Mshirikishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon na kuongeza kuwa, hatua ya nchi hizo kuyatumia makundi ya kigaidi kufikia ajenda zao, itazitumbukia nyongo.

Hussein Jaberi Ansari amesema yumkini nchi hizo zikafikia maslahi na manufaa ya muda mfupi lakini jambo ambalo halina shaka ni kwamba, kitendo hicho kitakuwa na taathira hasi kwa nchi hizo katika siku za baadaye.

Sigrid Kaag, Mshirikishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon

Akiashiria karata inayochezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika nchi za Lebanon na Syria, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kitendo cha Tel Aviv kuyapa misaada ya kimatibabu makundi ya kigaidi na kitakfiri katika nchi mbili hizo zitagonga mwamba.

Wakati huo huo, Hussein Jaber Ansari, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekariri juu ya sera na msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu wa kuunga mkono usalama na uthabiti katika nchi ya Lebanon huku akizitaka pande husika katika nchi hiyo ya Kiarabu kusuluhisha tofauti zao.

Kwa upande wake, Sigrid Kaag, Mshirikishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon ameeleza matumaini ya kupatiwa ufumbuzi mgogoro wa kisiasa katika nchi hiyo ya Kiarabu, ambayo imekuwa bila rais tangu Mei mwaka 2014.