Zolfaghari: Marekani inafanya njama za kueneza harakati za Kiwahabi M/Kati
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i18289-zolfaghari_marekani_inafanya_njama_za_kueneza_harakati_za_kiwahabi_m_kati
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Iran, Hossein Zolfaghari amesema kuwa, hivi sasa Marekani inafanya njama za kueneza harakati za makundi ya ukufurishaji ya Kisalafi ndani ya nchi za Iran, Pakistan na Afghanistan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 28, 2016 01:02 UTC
  • Zolfaghari: Marekani inafanya njama za kueneza harakati za Kiwahabi M/Kati

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Iran, Hossein Zolfaghari amesema kuwa, hivi sasa Marekani inafanya njama za kueneza harakati za makundi ya ukufurishaji ya Kisalafi ndani ya nchi za Iran, Pakistan na Afghanistan.

Zolfaghari ambaye pia ni mkurugenzi wa masuala ya usalama na kijeshi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran ameyasema hayo mjini Qum katika kongamano la 'Wabeba ujumbe wa Arubaini ya Imam Hussein AS'  na mbali na kuashiria mabadiliko yanayojiri hivi sasa katika eneo la Mashariki ya Kati amesema kuwa, hivi sasa Marekani na waitifaki wake wa Magharibi kwa kushirikiana na nchi kadhaa za Kiarabu, inafanya njama chafu za kueneza harakati za makundi ya ukufurishaji katika maeneo ya mashariki mwa Iran na pia katika nchi jirani za Pakistan na Afghanistan.

Hossein Zolfaghari, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Iran

Amesema kuwa hivi sasa maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wanafanya kila wawezalo ili kupotosha mafundisho sahihi ya madhehebu ya Kishia na kuzusha mizozo na mifarakano baina ya Waislamu. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Iran ameelezea juhudi kubwa za viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu kwa ajili ya kustawisha miundombinu na kuboresha huduma kwa wafanya ziara ya Arubaini ya Imam Hussein AS huko Karbala mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana na kusema kuwa, uchunguzi uliofanywa unaonyesha kuweko maboresho makubwa katika uwanja huo.

Magaidi wa Kiwahabi wa ISIS

Ameongeza kuwa, kwa mujibu wa ushirikiano uliopo baina ya Iran na Iraq, raia wa kigeni waishio humu nchini, wanaweza kuchukua viza kwa njia nyepesi kwa ajili ya kushiriki katika Arubaini ya Imam Hussein AS huko Karbal, Iraq.