Spika wa Bunge la Iran asisitiza kustawishwa uhusiano na nchi za Kiislamu
(last modified Mon, 14 Nov 2016 04:08:23 GMT )
Nov 14, 2016 04:08 UTC
  • Spika wa Bunge la Iran asisitiza kustawishwa uhusiano na nchi za Kiislamu

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema Iran inachukua hatua kwa lengo la kustawisha uhusiano wa pande zote na nchi za Kiislamu na za Kiarabu

Ali Larijani ameyasema hayo mjini Tehran katika mazungumzo na Khudhair Al-Khazai, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Chama cha Ad-Da'wah cha Iraq ambapo mbali na kusisitizia udharura wa kuwa na mtazamo chanya baadhi ya nchi za eneo la Mashariki ya Kati amesisitiza kuwa kuweko Iraq yenye amani na uthabiti ni miongoni mwa matakwa ya wananchi na viongozi wa Iran.

Spika wa Bunge la Iran ameashiria ushindi wa karibuni wa vikosi vya Iraq dhidi ya magaidi wa kitakfiri na kusisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kusaidia ustawi na maendeleo ya Iraq kwa kuipatia nchi hiyo uzoefu na tajiriba yake katika nyuga za kiuchumi, kisiasa, kielimu na kiutamaduni.

Kwa upande wake Khudhair Al-Khazai, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Chama cha Ad-Da'wah cha Iraq ambaye alikuwa pia makamu wa rais wa zamani wa Iraq amesema, Iran na Iraq zina uhusiano imara unaozingatia hali ya kuheshimiana na manufaa ya pande mbili.

Vikosi vya Iraq vikiendelea na operesheni za kuukomboa mji wa Mosul

Al-Khazai amezungumzia pia kutimuliwa baada ya muda si mrefu ujao magaidi wote wa kundi la kitakfiri katika mji wa Mosul na kuongeza kuwa: Vikosi vya ulinzi vya Iraq vikiwa bega kwa bega na vikosi vya kujitolea vya wananchi vingali vinapambana vikali na makundi ya kigaidi nchini humo.

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Chama cha Ad-Da'wah ameshukuru pia misaada athirifu ya Iran kwa ajili ya kurejesha uthabiti na utulivu nchini Iraq.../  

Tags