Dakta Larijani: Uungaji mkono kwa magaidi unafanyika kutelekeza malengo ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i22786-dakta_larijani_uungaji_mkono_kwa_magaidi_unafanyika_kutelekeza_malengo_ya_israel
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, himaya na uungaji mkono wa baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati kwa magaidiunafanyika kwa ajili ya kutekeleza malengo ya utawala haramu wa Israel.
(last modified 2026-01-14T11:42:18+00:00 )
Jan 04, 2017 04:14 UTC
  • Dakta Larijani: Uungaji mkono kwa magaidi unafanyika kutelekeza malengo ya Israel

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, himaya na uungaji mkono wa baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati kwa magaidiunafanyika kwa ajili ya kutekeleza malengo ya utawala haramu wa Israel.

Dakta Ali Larijani amesema hayo katika mazungumzo yake hapa mjini Tehran na Nouri al-Maliki, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iraq na kukosoa hatua ya baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati ya kuzusha migogoro katika eneo hili kupitia himaya na uungaji mkono wao kwa makundi ya kigaidi.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia matukio ya Iraq katika mazungumzo yake na Nouri al-Maliki na kubainisha kwamba, umoja na maafikiano ya kitaifa baina ya makundi tofauti ya kisiasa ya Iraq ndio siri ya mafanikio ya nchi hiyo katika kupambana na ugaidi.

Nouri al-Maliki, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iraq

Dakta Larijani amebainisha kuwa, kuimarishwa mshikamano na mwafaka wa kitaifa wa jumla na kuondolewa hitilafu baina ya mirengo mbali mbali ya kisiasa ya iraq ni jambo ambalo linaweza kupiga jeki juhudi za kuyapatia ufumbuzi matatizo ya wananchi wa nchi hiyo.

Kwa upande wake Nouri al-Maliki Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iraq ameisifu misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na masuala mbalimbali ya Mashariki ya Kati hususan migogoro wa Iraq na Syria na kusema kuwa,  daima sera za Iran zimekuwa ni kuunga mkono muqawama na mapambano ya kweli dhidi ya ugaidi.