Zarif: Iran inapinga ushiriki wa Marekani katika mazungumzo ya Astana kuhusu Syria
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i23794-zarif_iran_inapinga_ushiriki_wa_marekani_katika_mazungumzo_ya_astana_kuhusu_syria
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Muhammad Javad Zarif amesema kuwa, Tehran inapinga ushiriki wa Marekani katika mazungumzo ya stana, mji mkuu wa Kazakhstan kuhusiana na Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 18, 2017 03:54 UTC
  • Zarif: Iran inapinga ushiriki wa Marekani katika mazungumzo ya Astana kuhusu Syria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Muhammad Javad Zarif amesema kuwa, Tehran inapinga ushiriki wa Marekani katika mazungumzo ya stana, mji mkuu wa Kazakhstan kuhusiana na Syria.

Zarif ameyasema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na Shirika la Habari la TASNIM juu ya uwezekano wa kushirikishwa Marekani katika kikao cha mazungumzo ya amani ya Syria mjini Astana na kuongeza kuwa, Iran haikuialika Marekani kama ambavyo pia haitaki nchi hiyo ishiriki kikao hicho.

Sargey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia

Kabla ya hapo Sargey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia aliwambia waandishi wa habari kwamba, anadhani kuialika serikali mpya ya Donald Trump, rais mteule wa Marekani katika mazungumzo hayo ya amani ya Syria ni suala sahihi. Mazungumzo ya amani ya Syria baina ya wapinzani wabeba silaha na serikali ya Rais Bashar al-Assad kwa upatanishi wa Iran, Russia na Uturuki yamepangwa kufanyika tarehe 23 ya mwezi huu mjini Astana.

Rais Bashar al-Assad wa Syria

Ni vyema kuashiria kuwa, mazungumzo hayo yamekuja ikiwa ni baada ya kushindwa makundi ya kigaidi na waungaji  mkono wao ikiwemo Marekani, Saudia na Uturuki huko katika mji wa Aleppo, kaskazini mwa Syria sanjari na kukubali usitishaji vita wa nchi nzima.