Shamkhani: Iran imedhamiria kufuatilia ufumbuzi wa kisiasa kwa ajili ya Syria
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i24729-shamkhani_iran_imedhamiria_kufuatilia_ufumbuzi_wa_kisiasa_kwa_ajili_ya_syria
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuhusu wasiwasi walionao viongozi wa baadhi ya nchi za eneo hili kuhusu ubunifu wa kisiasa wa pande tatu za Iran, Russia na Uturuki kwamba wasiwasi huu unatokana na kudhoofika makundi ya kigaidi.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Feb 05, 2017 10:43 UTC
  • Shamkhani: Iran imedhamiria kufuatilia ufumbuzi wa kisiasa kwa ajili ya Syria

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuhusu wasiwasi walionao viongozi wa baadhi ya nchi za eneo hili kuhusu ubunifu wa kisiasa wa pande tatu za Iran, Russia na Uturuki kwamba wasiwasi huu unatokana na kudhoofika makundi ya kigaidi.

Alexander Lavrentiev Mjumbe Maalumu wa Rais wa Russia katika masuala ya Syria ambaye yuko ziarani hapa Tehran, leo Jumapili amekutana na Ali Shamkhani Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran na kujadili matukio ya hivi karibuni huko Syria, katika eneo la Mashariki ya Kati na kuhusu ushirikiano wa pamoja na vita dhidi ya ugaidi. 

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, (kulia) katika mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Russia katika masuala ya Syria (kushoto)

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesisitiza katika mazungumzo hayo kuwa, Jamhuri ya Kiislamu imedhamiria kufuatilia na kuupatia  ufumbuzi wa kisiasa mgogoro wa Syria ili kuhitimisha mgogoro huo na kwamba inaamini kuwa, njia ya utatuzi wa kijeshi pekee ndiyo inayofaa mbele ya makundi ambayo hayako tayari kuweka chini silaha. Shamkhani ameongeza kuwa suluhisho la kisiasa na la amani kwa ajili ya Syria na eneo hili halitaweza kufikiwa iwapo makundi ya kigaidi ya Daesh na al Nusra yataendelea kuwepo huko Syria  na kuungwa mkono kwa hali na mali na baadhi ya nchi za eneo. 

 Kwa upande wake Alxander Lavrentiev  ameunga mkono nafasi chanya ya Iran katika mchakato wa kisiasa wa kurejesha amani huko Syria na kueleza kuwa, kufanyika vyema kikao cha Astana ni mafanikio makubwa katika kuendeleza  ubunifu wa pande  tatu za Iran, Russia na Uturuki.