Zarif ajibu madai ya Netanyahu, historia ya Israel imejaa ukatili
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i25290-zarif_ajibu_madai_ya_netanyahu_historia_ya_israel_imejaa_ukatili
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu madai yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuhusu mipango ya kujihami ya makombora ya Iran.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Feb 18, 2017 01:11 UTC
  • Zarif ajibu madai ya Netanyahu, historia ya Israel imejaa ukatili

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu madai yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuhusu mipango ya kujihami ya makombora ya Iran.

Dakta Muhammad Javad Zarif amesema kuwa, utawala pekee wenye silaha za nyuklia na mabomu ya kuvuka mabara katika Mashariki ya Kati ambao pia historia yake imejaa uvamizi na ukatili sasa unatumia zana halali za kujihami za Iran kama wenzo wa kueneza propaganda zake chafu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Siku chache zilizopita Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu alidai katika kikao cha waandishi wa habari akiwa pamoja na Rais Donald Trump wa Marekani kwamba, miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia ya Iran na majaribio ya makombora ya Jamhuri ya Kiislamu ni tishio kwa usalama wa Israel na Marekani.

Netanyahu na Trump

Madai hayo ya Netanyahu pia yamejibiwa na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ambaye alisema juzi kuwa, maghala ya silaha za nyuklia ya utawala haramu wa Israel ndio tishio kubwa zaidi kwa amani na usalama wa dunia. 

Bahram Qasemi ameashiria madai yasiyo na msingi yaliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu dhidi ya miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia nchini Iran na kusema: Israel ina mamia ya mabomu ya nyuklia katika maghala yake na inahesabiwa kuwa tishio kubwa zaidi la usalama na amani ya Mashariki ya Kati na dunia nzima.

Bahram Qasemi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, matamshi ya Donald Trump na Benjamin Netanyahu katika mkutano wa waandishi wa habari hayana jipya isipokuwa kukariri madai yasiyo msingi wala thamani yoyote kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran.

Amesema madai hayo yanapingana na ripoti za mara kwa mara za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki zilizothibitisha kuwa miradi ya nyuklia ya Iran inafanyika kwa malengo ya amani.