Iran na Oman zaanza maneva ya uokoaji katika lango la Hormuz
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i27584-iran_na_oman_zaanza_maneva_ya_uokoaji_katika_lango_la_hormuz
Vikosi vya majini vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Oman vimeanza maneva ya pamoja ya utafutaji na uokoaji katika maeneo ya mashariki ya Lango la Hormuz na katika maeneo ya kaskazini mwa Bahari ya Hindi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 10, 2017 09:11 UTC
  • Iran na Oman zaanza maneva ya uokoaji katika lango la Hormuz

Vikosi vya majini vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Oman vimeanza maneva ya pamoja ya utafutaji na uokoaji katika maeneo ya mashariki ya Lango la Hormuz na katika maeneo ya kaskazini mwa Bahari ya Hindi.

Admeri Habibullah Sayari Kamanda wa jeshi la majini la Iran amewaambia waandishi wa habari hii leo kuwa Jamhuri ya Kiislamu na Oman zinafanya maneva hiyo ya pamoja kila mwaka na kwamba nchi hizo mbili zimekuwa zikiendesha maneva hayo kwa kupokezana. Kamanda wa jeshi la majini la Iran Admeri Habibullah Sayyari amesema Oman ndiye mwenyeji wa maneva hii ya mwaka huu.

Maneva ya utafutaji na uokoaji ya Iran na Oman katika lango la Hormuz 

Ameongeza kuwa meli tatu na helikopta moja zinashiriki kwenye maneva hayo yaliyokusudiwa kuimarisha usalama katika eneo. Hadi kufikia sasa Iran na Oman zimeshafanya maneva kadhaa za utafutaji na uokoaji kwa lengo la kujiweka tayari kutoa huduma, kutekeleza oparesheni za uokoaji, kuimarisha kiwango cha ushirikiano wa kikanda na kubadilishana uzoefu. Wakati huo huo Admeri Habibullah Sayyari amesema kuwa vikosi vya majini vya Iran na Pakistan vinapanga kufanya maneva ya mbinu hapo kesho.