Zarif: Wananchi wa Iran hawaogopeshwi na vitisho
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i29598-zarif_wananchi_wa_iran_hawaogopeshwi_na_vitisho
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, taifa la Iran ni taifa imara na la watu wasiotetereka hivyo haliogopeshwi na vitisho vyovyote vya Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 25, 2017 23:25 UTC
  • Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran
    Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, taifa la Iran ni taifa imara na la watu wasiotetereka hivyo haliogopeshwi na vitisho vyovyote vya Marekani.

Waziri Mohammad Javad Zarif alisema hayo jana hapa mjini Tehran na kusisitiza kuwa, kujitokeza kwa wingi wananchi wa Iran katika medani mbalimbali za kumkatisha tamaa adui kama vile katika uchaguzi wa hivi karibuni wa Mei 19 kwa uongozi wa busara wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kumesafisha vumbi lote la uongo, tuhuma na uenezaji wa chuki dhidi ya Iran.

Uchaguzi nchini Iran, kigezo ni kura za wananchi

 

Amesema, taifa la Iran limeionesha dunia kuwa inabidi kuwaheshimu wananchi wa Iran na kuachana na lugha za vitisho na udhalilishaji dhidi yao.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa, wananchi wa Iran hawana haja na nasaha wala idhini ya mtu yeyote katika kujidhaminia usalama, uhuru, maendeleo na ustawi wao wa kisayansi na kiteknolojia, bali wanategemea wataalamu wao wenyewe kujidhaminia mambo hayo.