Jul 02, 2017 08:10 UTC
  • Mkutano wa kimataifa wa

Kongamano la Kimataifa la Marekani, Haki za Binadamu na Ubeberu limeanza mapema leo mjini Tehran likihudhuriwa na wataalamu wa hapa nchini na kutoka nje ya nchi nchi.

Kongamano hilo linafanyika kwa ushirikiano wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Dunia ya Iran, Jumuiya ya Kiislamu ya Haki za Binadamu ya London na Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Dunia.

Washiriki katika kongamano hilo la kimataifa wanajadili hali ya haki za binadamu nchini Marekani.

Jumuiya mbalimbali za haki za binadamu zimekuwa zikiilaumu Marekani na washirika wake wa kimagharibi kuwa zinakiuka haki za binadamu na wakati huo huo zikijinadi kuwa washika bendera ya kutetea haki hizo. 

Watoto wa Yemen wanaendelea kuuawa kwa silaha za Marekani

Ukiukaji wa haki za binadamu umekithiri na kuvuka mpaka nchini Marekani baada ya kushika hatamu za uongozi wa nchi hiyo Donald Trump ambaye amekuwa akipendekeza sheria zinazowabana wahajiri na wageni hususan Waislamu.   

Tags