Dakta Zarif aitaka Marekani iangalie upya misimamo yake kuhusu JCPOA
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i31736-dakta_zarif_aitaka_marekani_iangalie_upya_misimamo_yake_kuhusu_jcpoa
Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya Iran na madola sita makubwa duniani ni yalikuwa makubaliano kimataifa na kwamba, Marekani inapaswa kuangalia upya misimamo yake kuhusiana na makubaliano haya ya kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 13, 2017 22:46 UTC
  • Dakta Zarif aitaka Marekani iangalie upya misimamo yake kuhusu JCPOA

Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya Iran na madola sita makubwa duniani ni yalikuwa makubaliano kimataifa na kwamba, Marekani inapaswa kuangalia upya misimamo yake kuhusiana na makubaliano haya ya kimataifa.

Dakta Muhammad Javad Zarif amesema hayo baada ya kuwasili mjini New York katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa na kusisitiza kwamba, makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi tano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA), ni maafikiano ya kimataifa ambayo yalifikiwa baada ya juhudi na mazungumzo ya miaka kadhaa.

Amesema kuwa, Iran inataraji kuziona pande nyingine husika katika makubaliano hayo zikiheshimu makubaliano hayo na kuyatekeleza kikamilifu kama zilivyoahidi katika hati ya maafikiano hayo.

Wawakilishi wa nchi zilizoshiriki katika mazungumzo ya nyuklia na Iran

Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inaamini kuwa, viongozi wa Marekani wanapaswa kuangalia upya misimamo yao kuhusiana na makubaliano ya nyuklia kwani kinyume na hivyo, makubaliano hayo hayawezi kudumu.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye ameelekea katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjinio New York anatarajiwa kushiriki katika mkutano wa umoja huo kuhusiana na masuala ya ustawi na maeandeleo.

Aidha akiwa mjini New York, Dakta Muhammad Javad Zarif anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo pambizoni mwa mkutano huo na shakhsia mbalimbali wa kimataifa.