Zarif aonya kuhusu kuibuliwa migogoro zaidi Mashariki ya Kati
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i36303-zarif_aonya_kuhusu_kuibuliwa_migogoro_zaidi_mashariki_ya_kati
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif ameonya kuhusu matokeo mabaya ya uchochezi zaidi wa migogoro katika eneo la Mashariki ya Kati.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Nov 10, 2017 11:30 UTC
  • Zarif aonya kuhusu kuibuliwa migogoro zaidi Mashariki ya Kati

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif ameonya kuhusu matokeo mabaya ya uchochezi zaidi wa migogoro katika eneo la Mashariki ya Kati.

Katika ujumbe alioundika Ijumaa katika ukurasa wake wa Twitter, Zarif ameashiria kuhusu kuhusika baadhi ya nchi katika kuunda makundi ya kigaidi ya ISIS au Daesh na Taliban na pia kuibua migogoro ya Yemen, Qatar na Lebanon na kusema: "Mtu mwenye uzoefu angeweza kubaini kuwa kuchochea migogoro zaidi si jambo la kiakili kwani hilo litaibua tu majuto siku za baadaye."

Baadhi ya nchi katika eneo, hasa Saudi Arabia, zimewekeza sana katika makundi ya kigaidi ili kufikia malengo yao haramu na hivyo nchi hizo zimekuwa na nafasi katika kuibua migogoro na mauaji ya watu wasio na hatia katika eneo.

Mrithi wa Kiti cha Ufalme Saudia Mohammad bin Salman amekuwa akichukua maamuzi yenye kuleta madhara Mashariki ya Kati

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza mara kadhaa kuwa, muelekeo uliojaa makosa na ulio na gharama kubwa kwa baadhi ya madola katika miaka ya nyuma haujakuwa na natija yoyote yenye manufaa. Kwa msingi huo madola hayo yenye kuibua migogoro yanapaswa kutumia busara na kuangalia uhalisia wa mambo katika eneo pasina kuwepo na taasubi au kiburi.