Ayatullah Araki: Lengo la Marekani ni kuvuruga irada ya taifa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i38301-ayatullah_araki_lengo_la_marekani_ni_kuvuruga_irada_ya_taifa
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu amesema: "Lengo la Marekani ni kuvuruga irada ya taifa la Iran."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 30, 2017 10:44 UTC
  • Ayatullah Araki: Lengo la Marekani ni kuvuruga irada ya taifa

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu amesema: "Lengo la Marekani ni kuvuruga irada ya taifa la Iran."

Ayatullah Muhsin Araki Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu ameyasema hayo leo alipohutubu kwa munasaba wa Siku ya Hamasa ya Tisa Dei (Disemba 30) katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA. Ayatullah Araki ameongeza kuwa adui afahamu kuwa njama, hadaa na fitina zake hazitavuruga irada ya taifa la Iran.

Ayatullah Araki ameongeza kuwa, taifa la Iran lina uzoefu wa maelfu ya miaka ya kupambana na wanaoibua fitina na hivyo litasimama kidete mbele ya Marekani na adui atapoteza matumaini katika njama zake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Leo Jumamosi tarehe 30 Disemba, inayosadifiana na tarehe 9 Dey kwa kalenda ya Kiirani, ni siku ya hamasa kubwa ya wananchi wa Iran ambayo ilivunja fitna kubwa ya mabeberu dhidi ya taifa la Kiislamu la Iran.

Mjumuiko wa Tisa Dey katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA mjini Tehran

Tarehe 9 Dey 1388 Hijria Shamsia iliyosadifiana na tarehe 30 Disemba 2009, mamilioni ya wananchi wa Iran katika kona zote za nchi walimiminika barabarani katika maandamano ya kupinga fitna kubwa iliyochochewa na mabeberu wa dunia waliotumia vibaya matokeo ya uchaguzi kufanya fujo katika mji mkuu wa Iran, Tehran.

Siku hiyo mamilioni kwa mamilioni ya wananchi wa Iran walijitolea kwa hali na mali kulinda misingi ya Uislamu na malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu, wakapaza sauti zao wakisema, kama adui ataendelea kufanya njama dhidi ya dini yao watasimama imara mbele ya dunia nzima kukabiliana naye.