Ayatullah Khatami: Adui anafanya njama za kulivunja moyo taifa la Iran
(last modified Fri, 26 Jan 2018 16:51:13 GMT )
Jan 26, 2018 16:51 UTC
  • Ayatullah Khatami: Adui anafanya njama za kulivunja moyo taifa la Iran

Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa njama za maadui wa Uislamu sasa zimeelekezwa katika mitandao ya kijamii na wanafanya jitihada za kulivunja moyo na kulikosesha matumaini taifa la Iran.

Ayatullah Ahmad Khatami ameyasema hayo leo katika hotuba za Swala ya Ijumaa ya mjini Tehran. Ameashiria njama na mipango ya adui dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kusisitiza kuwa: "Wamekosea wale wanaodhani kwamba maadui wa Umma wametupilia mbali mipango yao ya kuoindoa madarakani Jamhuri ya Kiislamu.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, hatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema miongoni mwa masharti ya kuendelea kuwepo Jamhuri ya Kiislamu ni kutekeleza maagizo na wasia wa hayati Imam Ruhullah Khomeini na kwamba kuna udharura wa kujifunza zaidi njia na fikra za Imam kwa Kiongozi wa sasa wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei.

Swala ya Ijumaa, Tehran

Ameyataja Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran kuwa ni neema kubwa ya Mwenyezi Mungu kwa Ulimwengu wa Kiislamu na kwamba mapinduzi hayo daima yanaandamana na jina la hayati Imam Khomeini.

Ayatullah Khatami pia ameashiria njama za hivi karibuni za maadui wa Uislamu hapa nchini na kusema taifa la Iran litajibu njama hizo kwa maandamano makubwa ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe tarehe 22 Bahman (11 Februari).