Zarif akosoa siasa za nchi za Magharibi kuhusu Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i42254-zarif_akosoa_siasa_za_nchi_za_magharibi_kuhusu_yemen
Sambamba na kuanza mwaka wa nne wa mapambano ya watu wa Yemen dhidi ya uvamizi na mashambulizi ya kila upande wa utawala wa kifalme wa SaudiA rabia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezikosoa nchi za Magharibi hususan Marekani kwa kuendelea kuuzia silaha utawala wa Aal Saud.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 26, 2018 22:00 UTC
  • Zarif akosoa siasa za nchi za Magharibi kuhusu Yemen

Sambamba na kuanza mwaka wa nne wa mapambano ya watu wa Yemen dhidi ya uvamizi na mashambulizi ya kila upande wa utawala wa kifalme wa SaudiA rabia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezikosoa nchi za Magharibi hususan Marekani kwa kuendelea kuuzia silaha utawala wa Aal Saud.

Muhammad Javad Zarif amesema katika ujumbe wake uliotumwa kwenye mtandao wa Tweeter kwamba: "Wakati baadhi ya nchi zikifurahia kukamua maziwa, zipo nchi nyingine zinazofurahia kukamuliwa." 

Dokta Zarif amesema kuwa, Wayemeni ambao baadhi ya wahalifu vijana wanataka kuwatumia kama ngazi ya kupanda juu, bado wamesahauliwa na nchi za Magharibi. 

Vita vya Saudi Arabia na washirika wake wanaosaidiwa na Marekani, Israel na nchi nyingine kadhaa vimeingia mwaka wake wa nne huku maelfu ya Wayemeni wakiendelea kuuawa hususan wanawake na watotro wadogo. 

Saudi Arabia inaendelea kuua raia wasio na hatia wa Yemen

Saudi Arabia na washirika wake waliivamia Yemen mwezi Machi mwaka 2015 kwa kisingizio cha kumrejesha madarakani kibaraka wa Riyadh, Abdrabbuh Mansur Hadi aliyetoroka nchi na kukimbilia Riyadh. 

Maelfu ya raia wa Yemen wameuawa na mamilioni ya wengine wamelazimika kuwa wakimbizi. Vilevile miundombinu muhimu ya nchi hiyo na taasisi za umma ikiwa ni pamoja na barabara kuu, viwanda, mahospitali, misikiti na mabwawa ya maji vimeharibiwa na ndege za kivita za Saudi Arabia.