Meja Jenerali Ghulam Ali Rashid: Tishio lolote litajibiwa vikali
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i46524-meja_jenerali_ghulam_ali_rashid_tishio_lolote_litajibiwa_vikali
Kamanda wa kamandi kuu ya Khatamul Anbiya (S.A.W) amesema kuwa vikosi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran viko imara na vimejiandaa kukabiliana na tishio lolote la makundi ya kigaidi na kitakfiri kuliko ilivyokuwa huko nyuma na kusisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itatoa jibu kali kwa tishio lolote dhidi yake.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 03, 2018 03:08 UTC
  • Meja Jenerali Ghulam Ali Rashid: Tishio lolote litajibiwa vikali

Kamanda wa kamandi kuu ya Khatamul Anbiya (S.A.W) amesema kuwa vikosi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran viko imara na vimejiandaa kukabiliana na tishio lolote la makundi ya kigaidi na kitakfiri kuliko ilivyokuwa huko nyuma na kusisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itatoa jibu kali kwa tishio lolote dhidi yake.

Akizungumza jana mbele ya hadhara ya makamanda wa kikosi cha majini cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mji wa Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran, Meja Jenerali Ghulam Ali Rashid Kamanda wa kamandi kuu ya Khatamul Anbiya (S.A.W) amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itayalinda kwa nguvu zote matunda ya usalama na uthabiti uliopo sasa katika eneo mkabala na vitisho vyovyote na njama za matakfiri na Wazayuni. 

Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, SEPAH

Meja jenerali Rashid aliendelea kusisitiza kuwa maadui wanafanya kila wawezalo kupitia vitisho ili kuathiri uwezo na irada ya wananchi wa Iran na mfumo wa Kiislamu na kwamba vitisho vya maadui vinapaswa kutambuliwa ili  kuweza kuvuka katika marhala hii  sawa kabisa na uzoefu wa miaka ya huko nyuma.