Majeshi ya Iran, Oman kushirikiana katika setka za tiba
Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran litashirikiana na Jeshi la Oman katika sekta ya tiba katika fremu ya ushirikiano wa kiulinzi wa nchi hizi mbili jinrani.
Hayo yamebainika katika mkutano wa Kamanda wa Masuala ya Afya na Mafunzo ya Tiba katika Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeri Daktari Mustafa Madah wakati alipokutana na Kaimu Mkuu wa Idara ya Afya na Tiba katika Jeshi la Oman Kanali Al-Harthy. Admeri Madah amesema kutembeleana jumbe za kitiba za majeshi ya nchi jirani ni kwa lango la kubadilishana tajiriba na uzoefu na ni jambo lenye umuhimu mkubwa. Amesema Iran iko tayari kuipa Oman uzeofu wake mkubwa katika nyuga zote za tiba ya kijeshi.
Admeri Madah ameongeza kuwa: " Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nafasi ya juu kimataifa katika uga wa tiba na iko tayari kutoa uzoefu na huduma kwa nchi nyingine."
Kwa upande wake Kanali Al Harthi Kaimu Mkuu wa Idara ya Tiba katika Jeshi la Oman amesema huduma za kiafya katika Majeshi ya Iran ni maarufu na kuongeza kuwa: "Oman inataka kuiga mfano wa Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uga wa tiba hasa uzoefu wa Iran katika sekta ya kutoa mafunzo na utafiti wa tiba.