Marekani yatoa vitisho tena kwa wanunuzi wa mafuta ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i47514-marekani_yatoa_vitisho_tena_kwa_wanunuzi_wa_mafuta_ya_iran
Serikali ya Marekani imezitishia tena kuziwekea vikwazo nchi zinazonunua mafuta kutoka Iran ikiwemo China.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 17, 2018 23:44 UTC
  • Marekani yatoa vitisho tena kwa wanunuzi wa mafuta ya Iran

Serikali ya Marekani imezitishia tena kuziwekea vikwazo nchi zinazonunua mafuta kutoka Iran ikiwemo China.

Brian Hook, ambaye ameteuliwa kuongoza kundi jipya liitwalo "Kundi la Uchukuaji Hatua Dhidi ya Iran" katika matamshi aliyotoa mara baada ya kushika wadhifa huo mpya amekariri vitisho vilivyotolewa huko nyuma na viongozi wengine wa Washington kwa kueleza kwamba: serikali ya Trump imeshajiandaa kuziwekea vikwazo nchi zote zitakazoendelea kununua mafuta ya Iran baada ya kumalizika muda wa mwisho uliowekwa wa mwezi Novemba, na kwamba vikwazo hivyo vitaijumuisha pia China ambayo ni mununuzi mkubwa zaidi wa mafuta ghafi ya Iran.

Hook ameongeza kuwa Marekani itatoa misamaha mbalimbali pia kwa baadhi ya nchi zitakazopunguza kiwango cha ununuzi wao wa mafuta kutoka Iran.

Mnamo tarehe 8 Mei, serikali ya Marekani ilichukua hatua ya upande mmoja na ya kinyume cha sheria ya kujitoa kwenye makubaliano ya kimataifa ya JCPOA sambamba na kutangaza kuwa itarejesha tena vikwazo vya nyuklia dhidi ya Iran katika awamu mbili za vipindi vya muda wa siku 90 na 180.

Hatua hiyo ya Washington ililalamikiwa na nchi mbalimbali duniani zikiwemo nchi tano zilizosaini pamoja na Marekani makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

China ni miongoni mwa nchi ambazo zimetangaza mara kadhaa kuwa hazina nia yoyote ya kufuata na kutekeleza vikwazo hivyo vya Marekani bali itaendelea kununua mafuta kutoka Iran.../