Zarif: Marekani ishtakiwe kwa jinai zake dhidi ya binadamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i49389-zarif_marekani_ishtakiwe_kwa_jinai_zake_dhidi_ya_binadamu
Waziri wa Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika radiamali yake kwa vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya watu wa Iran ameandika katika Twitter kuwa: "Marekani inapaswa kushtakiwa na kuwajibishwa kutokana na jinai zake dhidi ya binadamu".
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 09, 2018 04:25 UTC
  • Zarif: Marekani ishtakiwe kwa jinai zake dhidi ya binadamu

Waziri wa Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika radiamali yake kwa vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya watu wa Iran ameandika katika Twitter kuwa: "Marekani inapaswa kushtakiwa na kuwajibishwa kutokana na jinai zake dhidi ya binadamu".

Katika ujumbe wake huo mapema leo Ijumaa, Zarif ameandika: "Mike Pompeo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anabeba dhima ya vikwazo visivyo vya kisheria vya Washington dhidi ya Iran ambavyo vimewazuia watu wa Iran kupata huduma za kibenki kwa ajili ya kununua bidhaa za vyakula na dawa."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameendelea kubainisha kuwa: "Serikali ya Iran inakidhi mahitaji ya watu wake pamoja na kuwepo njama za Marekani lakini Marekani inapaswa kufikishwa kizimbani na kuwajibishwa kutokana na jinai zake dhidi ya binadamu."

Tarehe 8 Mei mwaka huu, rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kujitoa nchi yake kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kurejesha tena vikwazo vya nyuklia dhidi ya Iran. Awamu ya kwanza ya vikwazo hivyo ilianza kutekelezwa tarehe 7 Agosti, na awamu ya pili ilianza kutekelezwa rasmi Jumatatu ya tarehe 5 Novemba.