Iran yakosoa matamshi ya kiuhasma ya mshauri wa Trump
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i49500-iran_yakosoa_matamshi_ya_kiuhasma_ya_mshauri_wa_trump
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa matamshi ya dharau ya John Bolton Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Rais Donald Trump wa Marekani.
(last modified 2026-07-03T11:45:53+00:00 )
Nov 14, 2018 04:16 UTC
  • Iran yakosoa matamshi  ya kiuhasma ya mshauri wa Trump

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa matamshi ya dharau ya John Bolton Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Rais Donald Trump wa Marekani.

Bahram Qassemi Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema:  "Bolton ana tabia isiyo ya kawaida na anaugua ugonjwa  sugu wa 'kuinyanyasa Iran'.

Katika matamshi yake yaliyojaa uhasama hivi karibuni Bolton alisema Marekani itaishinikiza Iran hadi ihakikishe nchi hii inapata madhara makubwa. Qassemi amesema matamshi hayo ya kipuuzi ya Bolton yanaashiria utambulisho wake wenye chuki na hila wa kuwa dhidi ya watu wa Iran. 

Aidha amesema matamshi kama hayo hayatumiwi na wanasiasa wataalamu na wenye adhabu na kuongeza kuwa: "Si jambo la kustaajabisha kusikia maneno ya kipuuzi ya Bolton ambaye amekuwa na uhusiano na baadhi ya makundi ya kigaidi ambayo yamekuwa yakimpa pesa."

John Bolton

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: "John Bolton anapata furaha kamili, isiyo ya kawaida na inayoaibisha kuishinikiza, kuiwekea vikwazo na kuitisha Iran lakini hajaweza kuwadiriki watu wa Iran."

Qassemi amebaini kuwa, taifa la Iran leo kwa subira, stratejia na busara ya siku zote litasimama kidete mbele ya maadui na katu halitaruhusu ndoto zao za alinacha ziweze kutimia."