Apr 28, 2019 16:07 UTC

Mtaalamu mmoja wa ulimwengu wa Kiislamu kutoka Nigeria amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima iko mstari wa mbele katika kupigania umoja na mshikamano baina ya nchi za Kiislamu.

Sheikh Hassan Moumini amesema hayo leo pambizoni mwa Kongamano la Kimataifa la Mustakbali wa Ulimwengu wa Kiislamu hapa mjini Tehran na kuliambia shirika la habari la IRNA kwamba mchango wa Iran katika kudhamini usalama na amani ya eneo hili ni mkubwa na daima Tehran imekuwa ikipigania umoja na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu.

Mtaalamu huyo wa masuala ya ulimwengu wa Kiislamu aidha ameliambia shirika hilo la habari la IRNA kwamba Iran inadhamini pia manufaa ya nchi nyingine za Kiislamu kwa lengo la kulinda maslahi jumla ya Waislamu duniani.

Moja ya mikutano ya umoja wa Kiislamu mjini Tehran

 

Vile vile amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mwanachama muhimu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC na kusisitiza kuwa, Tehran haitetereki katika juhudi za kufanikisha malengo yake na muda wote inapigania umoja katika ulimwengu wa Kiislamu.

Kongamano la Kimataifa la Mustakbali wa Ulimwengu wa Kiislamu limeanza leo Jumapili hapa Tehran ilikihudhuriwa na wasomi na wataalamu kutoka nchi 10 za Kiislamu. Kongamano hilo la siku mbili linamalizika kesho Jumatatu.

Tags