Dehqan: Iran haitafanya mazungumzo yoyote na rais Trump wa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55600-dehqan_iran_haitafanya_mazungumzo_yoyote_na_rais_trump_wa_marekani
Mshauri wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran katika masuala ya sekta ya viwanda vya ulinzi amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu hataifanya mazungumzo na utawala wa sasa wa Marekani."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 25, 2019 21:11 UTC
  • Dehqan: Iran haitafanya mazungumzo yoyote na rais Trump wa Marekani

Mshauri wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran katika masuala ya sekta ya viwanda vya ulinzi amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu hataifanya mazungumzo na utawala wa sasa wa Marekani."

Brigedia Jenerali Hossein Dehqan Mshauri wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran katika sketa ya viwanda vya ulinzi ameyasema hayo katika mahojiano na Televisheni ya CBS ya Marekani ambapo ameashiria matamshi ya Rais Donald Trump wa Marekani kuwa angependea kufanya mazaunzumgo na viongozi wa Iran na kusema: "Iran ina shaka kubwa kuhusu nia ya Trump kwa sababu Marekani haikuheshimu mapatano ya nyuklia ya JCPOA ambayo yaliidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na ilijiondoa katika mapatano hayo."

Brigedia Jenerali Dehqan ambaye aliwahi kuwa waziri wa ulinzi wa Iran amekumbusha kuhusu vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran na kusema: "Wamarekani wanadhani kuwa, kwa vikwazo na kuwashinikiza wananchi wa Iran wanaweza kuibua ufa baina ya wananchi wa mfumo unaotawala, lakini uhasama wao huo sasa umepelekea kuwepo umoja na mshikamano zaidi baina ya wananchi na wakuu wa nchi."

Trump

Brigedia Jenerali Dehqan ameashiria, uwepo wa Marekani kijeshi katika eneo na muungano wake mpya wa jeshi la majini na kusema hatua hiyo ya Marekani itavuruga hali ya mambo katika Ghuba ya Uajemi. 

Mshauri wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran katika masuala ya sekta ya viwanda vya ulinzi pia amewatumia ujumbe watu wa Marekani na kusema: "Serikali ya Marekani inawatoza wananchi kodi na kulipa silaha na zana za kivita jeshi la nchi hiyo na kulitumia dhidi ya maslahi ya nchi na hatua hiyo imepelekea kuongezeka uhasama na chuki ya mataifa mengine duniani dhidi ya Marekani.