Dec 20, 2019 01:09 UTC
  • Ayatullah Makarim Shirazi: Mwisho wa uhai wa Uwahabi unakaribia

Ayatullah Nasir Makarim Shirazi mmoja wa Marja wakuu taqlidi katika mji mtakatifu wa Qum hapa nchini amesema kuwa Matakfiri wangeshatokomea kitambo kama kusingekuwepo na dola za mafuta na uungaji mkono wa Marekani kwa matakfiri hao.

Ayatullah Nasir Makarim Shirazi alisisitiza jana mbele ya wawakilishi wa Jumuiya ya Wanaharakati Wanaokosoa Uwahabi kwamba mwisho wa uhai wa Uwahabi umekaribia. Marja taqlidi huyo ameongeza kuwa hatari ya Uwahabi wa Kitakfiri haiishii tu kwa Waislamu na kuongeza kuwa Uwahabi umezaa ugaidi wa Daesh ambao ni hatari kwa wanadamu wote. 

Uwahabi unapaswa kupingwa kwa nguvu zote

Ayatullah Makarim Shirazi aidha ameashiria mtindo unaotumiwa na Mawahabi wa Kitakfiri wa kutumia kimaslahi baadhi ya Qurani Tukufu na kueleza kuwa: Mawahabi hukubali zile aya zinazokwenda sambamba na malengo na matakwa yao tu na kuweka kando zile zinazopinga matendo yao. 

Amesema jukumu la maulamaa ni kulinda dini na itikadi za watu wao. Ameongeza kwamba Mawahabi kwa kustafidi na baadhi ya madai yasiyo na msingi wanataka kuwapotosha walimwengu kuhusu Mashia na wafuasi wa Ahlul Bait wa Mtume (saw); jambo ambalo linahitajia kuwa macho kikamilifu. Akiendelea na hotuba yake mbele ya hadhara ya wanaharakati wanaokosoa Uwahabi, Ayatullah Makarim Shiraz ameongeza kusema kuwa, hivi sasa imekua rahisi sana kwa watu wengi kukabiliana na fikra za kitakfiri kwa kuzingatia kubainika wazi ukweli wa mambo kuhusiana na fikra hizo potofu. 

Tags