Ujerumani yakosoa mashinikizo ya kiwango cha juu ya Marekani dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i58626-ujerumani_yakosoa_mashinikizo_ya_kiwango_cha_juu_ya_marekani_dhidi_ya_iran
Baada ya kushika madaraka ya kuongoza Marekani, alianza kutekeleza siasa za kuiondoa nchi hiyo katika mikataba na makubakliano muhimu ya kimataifa, suala ambalo limekabilwia na malalamiko na upinzani ndani na nje ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 20, 2020 03:47 UTC
  • Heiko Maas
    Heiko Maas

Baada ya kushika madaraka ya kuongoza Marekani, alianza kutekeleza siasa za kuiondoa nchi hiyo katika mikataba na makubakliano muhimu ya kimataifa, suala ambalo limekabilwia na malalamiko na upinzani ndani na nje ya nchi hiyo.

Katika mkondo huo mwezi Mei mwaka 2018 Rais Donald Trump aliiondoa nchi hiyo katika makubalino ya nyuklia ya JCPOA na kuanza kutekeleza sera za mashinikizo ya kiwango cha juu kwa shabaha ya kuilazimisha Iran ikubali matakwa yake. Hatua hiyo imekabiliwa na upinzani mkubwa na hata kutoka kwa washirika wa Ulaya wa serikali ya Marekani.  

Katika uwanja huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas Jumapili ya jana alikosoa waziwazi sera na siasa za serikali ya Trump kuhusiana na Iran na kutahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea mgogoro mkubwa zaidi katika eneo la maghribi wa Asia. Mass ametoa wito wa kufanyika mazungumzo na Tehran. Sambamba na kukosoa sera za mashinikizo ya kiwango cha juu za Marekani dhidi ya Iran Heiko Maas anaamini kwa, vitisho na mashambulizi ya kijeshi havijabadili mienendo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran." Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani ameongeza kuwa: "Hatupaswi kudhani kwamba kubadilisha utawala nchini Iran kwa kutumia mashinikizo kunaweza kuboresha hali ya mambo. Mbinu kama hii haikuwa na matunda yaliyokusudiwa nchini Iraq.." Mass anasisitiza kuwa, ili kuboresha hali nchini Iran kuna udharura wa kufunguliwa milango na kufanya mazungumzo na Tehran. Amesisitiza kuwa vitisho na mashinikizo ya kijeshi haviwezi kuwa na matunda na kusema, Ulaya haitaki kushuhudia mgogoro mkubwa katika eneo la magharibi mwa Asia.

Heiko Maas

Ukosoaji huo mkali wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani dhidi ya siasa zilizojaa makosa na zilizofeli za serikali ya Donald Trump kuhusiana na Iran unaonesha kuwa, hata nchi za Ulaya waitifaki wa Marekani katika shirika la kijeshi la NATO zimeelewa kwamba, kung'ang'ania suala la kuendeleza siasa za mashinikizo ya kiwango cha juu si tu kwamba hakuwezi kutatua lolote, bali pia kunaweza kuwa na maafa makubwa kwa eneo zima la magharibi mwa Asia.

Serikali ya Donald Trump ilikuwa na matarajio kwamba, kwa kutumia mashinikizo ya kiwango cha juu itaweza kuiburuta Iran kwenye meza ya mazungumzo na kuilazimisha ikubali matakwa 12 ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo. Hata hivyo msimamo madhubuti wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu wa kukataa katakata matakwa haramu ya Marekani na kukataa kufanya mazungumzo na nchi hiyo vimeithibitishia serikali ya Trump kwamba, siasa za mashinikizo ya kiwango cha juu haziwezi kufua dafu.

Donald Trump

Nukta muhimu hapa ni kuwa, Ulya na Troika ya Ulaya  yaani nchi za Ujerumani, Uingereza na Ufaransa ambazo ni wanachama katika kundi la 4+1, licha ya kuelewa kwamba, siasa za za Washington dhidi ya Iran zimefeli lakini kivitendo zinaunga mkono siasa hizo badala ya kuishinikiza Marekani ili ibadili siasa zake kuhusiana na Iran. Katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu baada ya Marekani kujiondoa katika makubalino ya nyuklia ya JCPOA nchi hizo za Ulaya hazikuchukua hatua yoyote ya maana ya kupunguza athari mbaya za vikwazo vya upande mmoja vya serikali ya Washington dhidi ya Iran. Ni kutokana na hali hiyo ndipo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikaanza kutekeleza hatua tano za kupunguza utekelezaji wa vipengee vya makubaliano hayo. Kwa maneno mengine ni kuwa, kujiondoa Marekani kinyume cha sheria katika makubaliano hayo na kukataa au kushindwa nchi za Ulaya kutekeleza majukumu na ahadi zao ndivyo vilivyoilazimisha Iran ipunguze utekelezaji wa vipengee vya makubaliano hayo kwa mujibu wa vipengee nambari 26 na 36 vya JCPOA yenyewe. La kusikitisha zaidi ni kuwa, nchi za Ulaya sasa zimesalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani na zimeamua kuanzisha mchakato wa kutatua hitilafu ndani ya JCPOA unaofahamika kwa jina la 'Trigger Mechanism'.

Boris Johnson na Emmanuel Macron

Washington imekuwa ikitangaza kuwa, lengo la mashinikizo ya kiwango cha juu dhidi ya Iran ni kuilazimisha Tehran ikubali kuketi kwenye meza ya mazungumzo na kutupilia mbali mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kubuni mapatano mapya. Washington inadai kuwa, ili kufikia lengo hilo imetekeleza vikwazo ambavyo havijawahi kuonekana katika historia kwa shabaya ya kuipigisha magoti Iran na kuiburuta kwenye meza ya mazungumzo.

Akizungumzia vikwazo na mashinikizo hayo ya Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Muhammad Javad Zarif amesema kuwa vita vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya Iran ni ugaidi wa kiuchumi kwa sababu vinawalenga raia wa kawaida.

Pamoja na hayo yote Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza kuwa kamwe haitasalimu amri mbele ya ugaidi huo wa kiuchumi wa Marekani. Hii ni pamoja na kuwa, ripoti za taasisi za kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) zinasema kuwa, vikwazo vya upande mmoja vya Marekani vimefubaa na kwamba uchumi wa Iran utarejea katika mkondo wake wa kawaida katika mwaka huu wa 2020.