Maonyesho ya Kimataifa ya Gesi, Mafuta yaanza Tehran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i6430-maonyesho_ya_kimataifa_ya_gesi_mafuta_yaanza_tehran
Maonyesho ya 21 ya Kimataifa ya Gesi, Mafuta na Petrokemikali yameanza leo mjini Tehran ambapo kuna mashirika 1900 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi 38 za dunia.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 05, 2016 08:05 UTC
  • Maonyesho ya Kimataifa ya Gesi, Mafuta yaanza Tehran

Maonyesho ya 21 ya Kimataifa ya Gesi, Mafuta na Petrokemikali yameanza leo mjini Tehran ambapo kuna mashirika 1900 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi 38 za dunia.

Maoneysho hayo yamefunguliwa na maafisa wa ngazi za juu wa wizara ya mafuta ya Iran na ni ya kwanza kufanyika baada ya kutiwa saini mapatnao ya nyuklia baina ya Iran na madola sita makubwa duniani.

Maonyesho ya 21 ya Kimataifa ya Gesi, Mafuta na Petrokemikali yamehudhuriwa na mashirika 880 kutoka nchi 38 kama vile Ujerumani, Ukraine, China, Italia, Imarati, Armenia, Austria, Ubelgiji, Ufaransa, India, Malaysia, Uholanzi, Poland, Canada, Venezuela, Korea Kusini, Russia, Uhispani, Uturuki, Uingereza, Brazil, Japan, New Zealand, Ureno na matawi ya mashirika ya Marekani yaliyo barani Ulaya.

Mashirika makubwa yanayoshiriki ni kama vile Siemens la Ujerumani, Lukoil na Gazprom ya Russia ambayo kwa muda mrefu hayakushiriki maonyosho hayo kutokana na vikwazo.

Inakadiriwa kuwa hifadhi ya mafuta ghafi ya petroli ya Iran katika Ghuba ya Uajemi imefikia mapipa bilioni 100.

Aidha Iran ina hifadhi ya mita mraba bilioni 187 za gesi asilia katika Ghuba ya Uajemi ambapo hivi sasa ina uwezo wa kuchimba asilimia 75 ya gesi hiyo.