Kiongozi Muadhamu Kuhutubu kwa mnasaba wa Maulid ya Mtume Muhammad SAW
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i64368-kiongozi_muadhamu_kuhutubu_kwa_mnasaba_wa_maulid_ya_mtume_muhammad_saw
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei atahutubu kwa njia ya televisheni kwa mnasaba wa maadhimisho ya kukumbuka siku ya kuzaliwa (Maulid) Mtume Muhammad SAW na pia uzawa wa mjukuu wake, Imam Jaafar Swadiq AS.
(last modified 2026-02-05T12:50:29+00:00 )
Nov 01, 2020 11:42 UTC
  • Ayatullah Sayyid Ali Khamenei
    Ayatullah Sayyid Ali Khamenei

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei atahutubu kwa njia ya televisheni kwa mnasaba wa maadhimisho ya kukumbuka siku ya kuzaliwa (Maulid) Mtume Muhammad SAW na pia uzawa wa mjukuu wake, Imam Jaafar Swadiq AS.

Kwa mujibu wa taarifa, hotuba hiyo ya Jumanne Novemba 3 2020  itaanza saa nne na nusu asubuhi kwa wakati wa Tehran na saa nne asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki na itarushwa hewani na radio na televisheni za Jamhuri ya Kislamu ya Iran ikiwemo Press TV kwa lugha ya Kiingereza na Al Alam kwa lugha ya Kiarabu.

Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaamini kuwa Mtume Muhammad SAW alizaliwa 12 Rabiul Awwal nao Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaamini kuwa ni 17 Rabiul Awwal.

Kwa msingi huo, Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitangaza kipindi cha kuanzia tarehe 12 hadi 17 Rabiul Awwal kila mwaka kuwa ni Wiki ya Umoja kati ya Waislamu kote duniani. Wiki ya Umoja ni fursa nzuri ya kuzikurubisha nyoyo za Waislamu na kuimarisha umoja na mshikamano wao katika kukabiliana na maadui wa ulimwengu wa Kiislamu.