Wahadhiri wa vyuo vikuu wa Iran walaani kuvunjiwa heshima Mtume (saw)
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i64421-wahadhiri_wa_vyuo_vikuu_wa_iran_walaani_kuvunjiwa_heshima_mtume_(saw)
Wahadhiri wa vyuo vikuu nchini Iran wametoa taarifa wakilaani vikali hatua ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ya kumvujia heshima Mtume Muhammad (saw).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 04, 2020 03:35 UTC
  • Wahadhiri wa vyuo vikuu wa Iran walaani kuvunjiwa heshima Mtume (saw)

Wahadhiri wa vyuo vikuu nchini Iran wametoa taarifa wakilaani vikali hatua ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ya kumvujia heshima Mtume Muhammad (saw).

Taarifa iliyotolewa na wahadhiri wa vyuo vikuu vya Iran imesema kuwa, hatua ya kuaibisha ya Wafaransa ya kumvunjia heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kielelezo cha kueneza chuki na kuhujumu matukufu ya kidini, na vilevile ukiukaji wa uhuru wa kuabudu na uhuru wa kidini.

Wakati huo huo na sambamba na maadhimisho ya Maulidi na kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (saw), malenga wa Iran wamelaani vikali dharau na matusi ya jarida la Charlie Hebdo la Ufaransa ya kuchapisha vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) na hatua ya rais wa nchi hiyo ya kutetea kitendo hicho kiovu. Malenga hao wametoa wito wa kutumiwa nyenzo mbalimbali ikiwemo sanaa na mashairi kwa ajili ya kuzima njama za maadui.

Matamshi yaliyotolewa na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akidai kwamba Uislamu uko kwenye mgogoro duniani kote na msimamo wake wa kuunga makono kitendo kiovu cha jarida la nchi hiyo la Charlie Hebdo cha kuchapisha vikatuni vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW kimeughadhibisha Ulimwengu wa Kiislamu. Macrom ametangaza kuwa Ufaransa itaendelea kuchapisha vibonzo hivyo.

Maandamano makubwa yamefanyika na yanaendelea kufanyika katika nchi mbalimbali kulaani msimamo huo wa Macron. Mbali na maandamano, zinaendeshwa kampeni pia za kususia bidhaa za Ufaransa.