Kiongozi Muadhamu aomboleza kifo cha Ayatullah Misbah Yazdi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i65539-kiongozi_muadhamu_aomboleza_kifo_cha_ayatullah_misbah_yazdi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe maalumu wa kuomboleza kifo cha mwanachuoni mkubwa, faqihi mwanaharakati, Ayatullah Muhammad Taqi Misbah Yazdi.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Jan 02, 2021 03:58 UTC
  • Kiongozi Muadhamu aomboleza kifo cha Ayatullah Misbah Yazdi

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe maalumu wa kuomboleza kifo cha mwanachuoni mkubwa, faqihi mwanaharakati, Ayatullah Muhammad Taqi Misbah Yazdi.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe huo wa tanzia leo Jumamosi na sambamba na kutoa mkono wa pole kufuatia kifo cha mwanachuoni huyo mkubwa kwa familia yake, wanafunzi na wapenzi wake wote, amesema kwamba, Ayatullah Misbah Yazdi alikuwa ni mwanafikra mkubwa, kiongozi mwenye ustahiki, mwenye ufasaha wa lugha na imara katika kutangaza haki na kutotetereka katika njia iliyonyooka.

Ayatullah Khamenei aidha amesema kuhusu mchango mkubwa wa Ayatullah Misbah Yazdi kwamba kwa kweli alikuwa na sifa za kipekee katika kuzalisha fikra za kidini, kutunga vitabu muhimu sana, kulea wanafunzi bora na kuyapigania Mapinduzi ya Kiislamu kwa nguvu zake zote katika medani zote muhimu na nyeti.

Ayatullah Misbah Yazdi

 

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesema, imani thabiti ya kidini na taqwa ndizo sifa za daima alizokuwa nazo Ayatullah Misbah Yazdi tangu ujanani mwake hadi mwishoni mwa umri wake na alipata taufiki ya kupata mafanikio mazuri katika njia ya maarifa ya tawhidi ikiwa ni atia na zawadi kubwa ya Mwenyezi Mungu kwa mwanachuoni huyo mwanaharakati.

Ayatullah Muhammad Taqi Misbah Yazdi, mjumbe wa Baraza la Wanavyuoni Wataalamu linalomchagua na kusimamia kazi za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ambaye pia alikuwa mkuu wa Taasisi ya Elimu na Utafiti ya Imam Khomeini MA, alifariki dunia jana Ijumaa jioni, Januri 1, 2021, akiwa na umri wa miaka 85.