Iran yakosoa wanaotumia ugaidi kufikia malengo yao
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i6745-iran_yakosoa_wanaotumia_ugaidi_kufikia_malengo_yao
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa sera za baadhi ya nchi kutumia ugaidi kama chombo cha kufikia malengo yao katika eneo na kusema jambo hilo litakuwa na natija kinyume na inavotarajiwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 09, 2016 10:49 UTC
  • Iran yakosoa wanaotumia ugaidi kufikia malengo yao

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa sera za baadhi ya nchi kutumia ugaidi kama chombo cha kufikia malengo yao katika eneo na kusema jambo hilo litakuwa na natija kinyume na inavotarajiwa.

Hossein Jaberi Ansari, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran katika mkutano wa kila wiki na waandishi habaria mjini Tehran pia ameashiria tamko la Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa aliyesema milipuko ya kigaidi Iraq inatekelezwa na wanaotoka Uturuki. Ameongeza kuwa, hatua ya baadhi ya nchi kutumia makundi ya kigaidi si kwa maslahi ya nchi yoyote katika eneo bali jambo hilo litakuwa na matokeo mabaya.

Ansari ameongeza kuwa, Iran daima imekuwa ikitaraji kuwa nchi jirani na nchi za eneo hazitaruhusu makundi ya kigaidi yaweze kufanikiwa.

Kuhusu dola bilioni mbili za Iran ambazo hivi karibuni ziliziouliwa na mahakama nchini Marekani amesema, kuna kamati maalumu iliyobuniwa kufuatilia kadhia hiyo na tayari Rais wa Iran ameshakabidhiwa ripoti.