Mohsen Rezai: Daesh ni mdhamini wa usalama wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i7015-mohsen_rezai_daesh_ni_mdhamini_wa_usalama_wa_israel
Katibu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kushamiri na kuenea makundi ya kitakfiri na kigaidi kumevuruga amani ya eneo la Mashariki ya Kati na kudhamini usalama wa utawala wa Kizayuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 13, 2016 23:20 UTC
  • Mohsen Rezai: Daesh ni mdhamini wa usalama wa Israel

Katibu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kushamiri na kuenea makundi ya kitakfiri na kigaidi kumevuruga amani ya eneo la Mashariki ya Kati na kudhamini usalama wa utawala wa Kizayuni.

Mohsen Rezai, amesema kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh ni tunda la mmea wa Uistikbari na kufafanua kuwa kuenea na kushamiri makundi yenye misimamo ya kufurutu mpaka katika eneo, leo kumeiweka Israel katika mazingira bora kabisa ya kiusalama.

Katibu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, hujuma angamizi dhidi ya maelfu ya wanawake na watoto wa Yemen ni mfano hai wa ufufuaji zama zilizokuwa zimeshazikwa za ujahilia; na akafafanua kwamba, makundi ya kitakfiri na kigaidi yanafanya kila aina ya jinai kwa kutumia jina la Uislamu na kurejesha tena zama za ujahilia.

Sambamba na kusisitiza Waislamu kuwa macho na njama zilizopangwa na maadui wa dini, Mohsen Rezai amesema, maadui, ambao wamegonga mwamba katika vita vya kimfumo na kisiasa walivyoanzisha dhidi ya Iran, sasa wanafanya juu chini kupitia vikwazo na mashinikizo ya kiuchumi ili kuipigisha magoti Iran.

Amesema njia pekee ya kukabiliana na silaha ya kiuchumi ya adui ni kuzingatia na kuupa umuhimu Uchumi wa Muqawama.../