Zarif: Ushiriki wa wananchi katika uchaguzi kutasambaratisha pia vikwazo vya baadaye
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa kushiriki kwa wingi wananchi wa Iran katika uchaguzi si tu kutaharakisha kuondolewa vikwazo bali kutasambartisha pia vikwazo vya baadaye.
Muhammad Javad Zarif ameongeza kuwa, kushiriki kwa wingi wananchi katika uchaguzi si tu kuwa kutaharakisha kuondolewa vikwazo na kubomoa msingi wa vita vya kiuchumi dhidi ya taifa jasiri la Iran bali kutasambaratisha pia vikwazo vya baadaye.
Zarif ameashiria namna wananchi walivyo wadhamini wa uhuru, usalama, fakhari na maendeleo ya nchi na kueleza kuwa: kushiriki kwa wingi na kwa busara wananchi katika kuainisha mustakbali wao ndiko kunakoleta nguvu ya taifa, kunakopelekea kulindwa maslahi ya taifa kimataifa na ndio msingi mkuu katika maelewano ya kimataifa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: kuongezeka ushiriki wa wananchi katika uchaguzi kutawavunja moyo wachupaji mipaka, Wazayuni na magaidi wa kiuchumi ambao wameshindwa pakubwa kwa hatua zao za uhasama na kuzidisha kwao vikwazo dhidi ya Iran.
Duru ya13 ya uchaguzi wa Rais wa Iran imepangwa kufanyika tarehe 18 mwezi huu wa Juni sawa na tarehe 28 mwezi Khordad mwaka 1400 kwa kalenda ya Kiirani.