Khatibzadeh: Vikwazo vya Marekani inabidi viondolewe kwa sura inayohisika
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, vikwazo vya Marekani inabidi viondolewe kwa sura inayohisika akisisitiza kuwa, tayari hivi sasa matini za makubaliano ya kufufua mapatano ya nyuklia ya JCPOA zimeshakuwa ndefu na sehemu zinazohitajia kukamilishwa pia zipo lakini hali yake imeshajulikana.
Saeed Khatibzadeh alisema hayo jana mbele ya waandishi wa habari na kuongeza kuwa, kwa kuzingatia maendeleo mazuri yaliyofikiwa katika makublaiano ya kufufua mapatano ya JCPOA, na ingawa yako baadhi ya mambo yatujaafikiana, lakini lililo muhimu ni kwamba mambo tuliyokubaliana ni mengi zaidi ikilinganishwa na yale ambayo bado hayajatatuliwa.
Pande zote zinazoshiriki katika mazungumzo ya Vienna zinakiri kwamba tumefikia mahala pazuri katika mazungumzo hayo na kila mmoja anaonesha waziwazi nia ya kweli ya kufikia kwenye makubaliano ya kufufua JCPOA.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran vile vile amesema, jambo ambalo linakubaliwa na kila mtu humu nchini ni mosi, vikwazo vya Marekani lazima viondolewe kwa sura inayoonekana; na pili, kusiingizwe jambo lolote lililo nje ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza mara chungu nzima kwamba mara tu mapatano ya JCPOA yatakapoanza kutekelezwa kikamilifu yna pande zilizofikia makubaliano hayo na Tehran, Jamhuri ya Kiislamu nayo itarejea kutekeleza kikamilifu vipengee vyote baada ya kujiridhisha kuwa pande nyingine zinayaheshimu vilivyo makubaliano hayo ya kimataifa.
Akijibu swali kuhusu hali ya Lebanon na uundwaji wa serikali ya nchi hiyo, Khatibzadeh amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalihesabu suala hilo kuwa ni la ndani ya Lebanon, na ni Walebanon wenyewe ndio pekee wenye haki ya kujiamulia mambo yao bila ya kuingiliwa na yeyote. Tehran inaheshimu maamuzi ya Walebanon na inatamani kuona serikali ya nchi hiyo inaundwa haraka iwezekanavyo.