Safari ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Armenia mjini Tehran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i75414-safari_ya_waziri_wa_mashauri_ya_kigeni_wa_armenia_mjini_tehran
Ararat Samveli Mirzoyan, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Armenia amekutana na kufanya mazungumzo hapa mjini Tehran na Hussein Amir-Abdollahian Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2026-08-11T03:40:48+00:00 )
Oct 05, 2021 06:53 UTC
  • Safari ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni  wa Armenia mjini Tehran

Ararat Samveli Mirzoyan, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Armenia amekutana na kufanya mazungumzo hapa mjini Tehran na Hussein Amir-Abdollahian Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ararat Samveli Mirzoyan, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Armenia aliwasili Jumatatu ya jana hapa mjini Tehran kwa safari rasmi ya kikazi inayolenga kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Katika mazungumzo yao na waandishi wa habari hapa mjini Tehran hiyo jana, mawaziri hao walisisitiza juu ya kuimarishwa uhusiano wa pande mbili. Amir-Abdollahina amesema kuwa, uhusiano wa Iran na Armenia ni mzuri na upo katika hali ya kukua zaidi siku baada ya siku.

Sambamba na kuendelea mvutano baina ya Azerbaijan na Armenia baada ya kutiwa saini hati ya makubaliano ya amani ya Karabakh, viongozi wa serikali ya Yerevan wameazimia kufanya mazungumzo zaidi na mataifa jirani kwa minajili ya kustawisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara.

Hapana shaka kuwa, moja ya yaliyokuwa malengo ya Nikol Pashnyan, Waziri Mkuu wa Armenia ya kutia saini Hati ya Amani ya Karabakh kwa upatanishi wa Russia ni kuhitimisha matatizo ya kimaisha ya wananchi wa nchi hiyo na hivyo kuzuia kuhajiri vijana wa Kiarmenia kuelekea katika mataifa mengine. Wakati huo huo, katika kipindi cha karibu mwaka mmoja uliopita, Nikol Pashinyan amefanya juhudi kubwa za kudhamini sehemu ya matakwa ya wananchi wa Armenia kupitia kuwa na uhusiano nchi yake na Azerbaijan pamoja na Uturuki.

Mazungumzo na Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na Armenia (Tehran 04.10.2021)

 

Hata hivyo kufanyika manuva ya pamoja ya kijeshi ya Jamhuri ya Azerbaijan na Uturuki katika eneo la mpaka wa Armenia kumewafanya viongozi wa Yerevan waingiwe na shaka juu ya kuweko njama mpya dhidi ya nchi yao.

Ukweli ambao haupaswi kupuuzwa ni huu kwamba, baada ya mapigano ya mpakani ya Aprili 2016, viongozi wa Armenia wamekuwa yakiyahesabu manuva ya kijeshi ya pamoja ya Azerbaijan na Uturuki kuwa yanakinzana na maslahi ya kitaifa ya nchi hiyo. Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana Ararat Mirzoyan, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Armenia badala ya kuimarisha uhusiano na Azerbaijan na Uturuki ameshajiika zaidi kuimarisha ushirikiano na Iran na Russia.

Na ndio maana Ararat Mirzoyan, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Armenia amefanya safari hapa Tehran. Ajenda kuu za mazungumzo yake na maafisa na viongozi mbalimbali wa Iran katika safari yake ya siku mbili hapa Tehran ni kujadilia masuala ya pande mbili na matukio ya hivi karibuni katika eneo la Asia Magharibi.

Kabla ya safari hiyo, wachambuzi wa mambo wa Kiarmenia walisema katika tathmini zao kuhusiana na safari ya Ararat Mirzoyan, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Armenia mjini Tehran kwamba, ushirikiano wa Tehran na Yerevan katika masuala mbalimbali hususan bidhaa zinazosafirishwa una umuhimu mkubwa na wa aina yake. Kwa mfano Gagik Aghajanyan, mchambuzi wa masuala ya kiuchumi na bidhaa zinazosafirishwa na mmoja wa maafisa wa kitengo cha usafirishaji na uchukuzi nchini Armenia anasema: Muelekeo wa bidhaa za biashara zinazosafirishwa za nchi hiyo kupitia Jamhuri ya Azerbaijan siyo jambo lenye faida kwa Yerevan.

 

Mchambuzi huyo wa masuala ya kiuchumi ameashiria hitilafu na mizozo yenye historia kongwe kati ya Yerevan na Baku na kubainisha kwamba, katika mazingira kama haya, haiwezekani kuwa na matumaini na muelekeo unaofaa kwa bidhaa zinazosafirishwa za Armenia kupitia Azerbaijan baada ya kuanzishwa njia ya chini kwa chini inayoendelea kujengwa huko Georgia na hivyo kuwekeza biashara kwa kutegemea njia hiyo.

Kupitia matamshi haya ya mchambuzi huyu mtajika wa Armenia inafahamika wazi kwamba, viongozi wa serikali ya Yerevan wanatoa uzingatiaji maalumu kwa ushirikiano wao na Tehran hususan katika masuala ya usafirishaji na uchukuzi wa bidhaa za biashara. Katika mazingira haya inapasa kusema kuwa, kuweko uhusiano mzuri baina ya Iran na Armenia katika miaka ya baada ya uhuru wa nchi hiyo mwaka 1991, uwanja wa kubadilisha utendaji wa nchi hiyo na kuuelekeza upande wa kushirikiana na Iran umeimarishwa siku baada ya siku.

Kimsingi ni kuwa, utendaji wenye uwiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mzozo wa Karabakh hususan katika mazingira ambayo Azerbaijan na Uturuki zilifunga mipaka yao na Armenia, ni jambo ambalo limeandaa uwanja wa kustawishwa zaidi uhusiano wa Tehran na Yerevan.

Ni vyemba kukumbusha hapa kuwa, Iran, Armenia, Georgia, Bulgaria na Ugiriki zilianza kufanya mazungumzo ya pande kadhaa mwaka 2016 kwa ajili ya kuanzisha korido ya usafishaji na uchukuzi ya mbalimbali atika njia ya Ghuba ya Uajemi-Bahari Nyeusi ambayo itaiunganisha Iran na Ulaya kupitia Armenia, Georgia na Bahari Nyeusi.

Bendera za Iran (kulia) na Armenia

 

Ushirikiano huu wa pande mbili na pande kadhaa unazidi kuimarika katika hali ambayo, Rais Ilham Aliyev wa Jamhuri ya Azerbaijan akitegemea ahadi za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel akishirikiana na baadhi ya viongozi wa Uturuki, anakusudia kutumia vibaya makubaliano yaliyofikiwa baada ya vita vya pili vya Karabakh na Armenia kwa ajili ya kubadilisha ramani ya jiopilitiki ya eneo la Caucasia Kusini.

Viongozi wa serikali ya Ilham Aliyev kama wanavyojidanganya ni kuwa, wanafanya juhudi za kuinyima Iran haki ya ujirani na Armenia. Hii ni katika hali ambayo, nchi mbili hizi jirani zimechukua hatua ya kuimarisha uhusiano wao katika nyanja zote kupitia uhusiano wao mwema na mzuri lengo hasa likiwa ni kusambaratisha njama za maadui wa mataifa yenye misimamo huru na yasiyokubali kuburuzwa. Safari ya sasa ya Ararat Mirzoyan, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Armenia  mjini Tehran inatathminiwa pia katika fremu hii.