Iran: Tuna nia ya kutaka kufikiwa makubaliano katika mazungumzo ya JCPOA
Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza tena leo kuwa, taifa hili linafuatilia ili kuhakikisha kwamba, kunapatikana makubaliano mazuri kupitia mazungumzo ya nyuklia ya Vienna Austria kati yake na kundii la 4+1.
Hussein Amir-Abdollahian amesema hayo leo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya na kusisitiza kwamba, Tehran ina nia ya dhati ya kutaka kufikiwa makubaliano katika mazungumzo hayo.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonya kuhusiana na mwenendo wa madola ya Ulaya wa kususua na kutotekeleza ahadi zao na jinsi madola hayo yasivyochukua hatua za maana hata katika duru hii ya mazungumzo ya nyuklia katika mji mkuu wa Austria Vienna.
Amir-Abdollahian ameongeza kuwa, mwaka uliopita yalisemwa mengi ya kutosha na kutolewa ahadi ambazo hazikutekelezwa, lakini leo umewadia wakati sasa wa kuchukuliwa hatua za kivitendo na Iran ina nia ya dhati na inafanya juhudi kwa ajili ya kufikiwa makubaliano.

Kwa upande wake, Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya ambaye pia ni mratibu wa mazunguumzo ya Vienna amesisitiza kuwa, Marekani na madola matatu ya Ulaya (Troika ya Ulaya) yamekumbushwa kwamba, mazungumzo ya Vienna yanapaswa kuangalia mambo kwa uhalisia wake na panbde mbili zihisi kupigwa hatua katikka mazungumzo hayo.