Iran: Uzayuni hauna nafasi katika mustakabali wa dunia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i78814-iran_uzayuni_hauna_nafasi_katika_mustakabali_wa_dunia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kulinda na kutetea haki, maslahi na ustawi wake kwa izza na mantiki; na kusisitiza kuwa utawala wa Kizayuni hauna nafasi katika mustakabali wa dunia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 04, 2022 04:39 UTC
  • Hossein Amir-Abdollahian
    Hossein Amir-Abdollahian

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kulinda na kutetea haki, maslahi na ustawi wake kwa izza na mantiki; na kusisitiza kuwa utawala wa Kizayuni hauna nafasi katika mustakabali wa dunia.

Hossein Amir-Abdollahian alisema hayo katika ujumbe aliotuma jana Jumatatu kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, akijibu matamshi ya kifidhuli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala bandia wa Israel, dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Amir-Abdollahian ameeleza kuwa, bwabwaja hizo za Wazayuni dhidi ya taifa kubwa la Iran ni mfano wa ndoto za Alinacha, na kwamba Uzayuni hauna nafasi yoyote katika mustakabali wa uliwengu.

Yair Lapid, Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala haramu wa Israel

Hivi karibuni, Yair Lapid, Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala haramu wa Israel alitoa matamshi ya uropokaji akidai kuwa Tel Aviv inaweza kulishambulia taifa la Iran ikilizimu, na wala haihitaji idhini ya utawala wa Rais Joe Biden wa Marekani ya eti kulinda usalama wake.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu italinda na kutetea haki na maslahi yake kwa nguvu zote, na kwamba utawala wa Kizayuni hauna nafasi katika mustakabali wa dunia.