Amir Abdollahian asisitiza kustawisha uhusiano na nchi za Kiafrika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i79608-amir_abdollahian_asisitiza_kustawisha_uhusiano_na_nchi_za_kiafrika
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza suala la kuimarisha uhusiano na nchi za Kiafrika na kustawishwa ushirikiano wa pande zote katika sekta mbalimbali kwa maslahi ya pamoja na nchi ya Togo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jan 25, 2022 15:04 UTC
  • Amir Abdollahian asisitiza kustawisha uhusiano na nchi za Kiafrika

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza suala la kuimarisha uhusiano na nchi za Kiafrika na kustawishwa ushirikiano wa pande zote katika sekta mbalimbali kwa maslahi ya pamoja na nchi ya Togo.

Hossein Amir-Abdollahian ameyasema hayo leo Jumanne hapa mjini Tehran katika mazungunzo yake na Robert Dussey, Waziri wa Mambo  ya Nje wa Togo. Amir Abdollahian ameeleza mafanikio ya Iran katika sekta mbalimbali na uwezo wa makampuni ya Kiirani katika nyanya za kiuchumi, kisayansi, kiteknolojia na afya. 

Vilevile ameashiria umuhimu wa viongozi wa nchi mbili kufanya ziara kwa lengo la kustawisha uhusiano wa pande mbili na kusisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kukuza ushirikiano na Togo. 

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Togo Bwana Robert Dussey amesema nchi yake ipo tayari kukuza uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hususan katika nyanja za biashara na uchumi. 

Tehran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Togo ameyaalika makampuni ya Iran kushiriki katika miradi ya maendeleo ya nchi yake ikiwemo miradi elimu, afya na nishati.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Togo pia wamekubaliana kuanzisha kamati ya pamoja ya kikazi, kuchunguza uwezekano wa kuanzisha balozi katika miji mikuu ya nchi mbili na kubadlishana jumbe za kibiashara.