Mazungumzo kuhusu kuondolewa Iran vikwazo vya kidhulma yanaendelea mjini Geneva
Mkuu wa timu ya Jamhuiri ya Kiislamu ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia, ameonana na mratibu wa kamati ya JCPOA mjini Geneva Uswisi.
Huo ni muendelezo wa awamu ya nane ya mazungumzo baina ya Iran na kundi la 4+1 ya kutafuta njia za kuondolewa vikwazo vya kidhulma ilivyowekewa Iran baada ya Marekani kujitoa kwenye mapatano hayo ya kimataifa, miaka kadhaa iliyopita.
Kwa mujibu wa Iran Press, Ali Bagheri-Kani mkuu wa timu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mazungumzo hayo ya Vienna ameonana na Enrique Mora mratibu wa mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kujadiliana naye masuala muhimu ya kuharakisha kufikiwa mapatano mazuri yaliyokusudiwa katika awamu ya nane ya mazungumzo hayo.
Kimsingi kumefanyika mazungumzo mawili huko Vienna, ya kwanza ni baina ya timu ya Iran na timu za nchi tatu za Ulaya za Ujerumani, Ufaransa na Uingereza na kikao hiki ambacho kimehudhuriwa na Ali Bagheri Khani mkuu wa timu ya Iran na Enrique Mora, mratibu wa makubaliano ya JCPOA.
Awamu ya nane ya mazungumzo ya Vienna kwa ajili ya kuiondolea Iran vikwazo vya kidhulma ilivyowekewa na Marekani, iliendelea tarehe 8 mwezi ulioisha wa Februari, yaani baada ya siku 11 za mapumziko ambapo timu za mazungumzo hayo zilirejea katika nchi zao kwa ajili ya mashauriano zaidi.