Iran: Ufaransa ndiyo inayovuruga zaidi mazungumzo ya nyuklia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i87600-iran_ufaransa_ndiyo_inayovuruga_zaidi_mazungumzo_ya_nyuklia
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amezungumzia mafanikio ya Iran katika uga wa teknolojia ya nyuklia na kusisitiza kuwa: Ufaransa ndiyo inayovuruga zaidi mazungumzo ya nyuklia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 30, 2022 03:30 UTC
  • Iran: Ufaransa ndiyo inayovuruga zaidi mazungumzo ya nyuklia

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amezungumzia mafanikio ya Iran katika uga wa teknolojia ya nyuklia na kusisitiza kuwa: Ufaransa ndiyo inayovuruga zaidi mazungumzo ya nyuklia.

Ameongeza kuwa, licha ya uvurugaji wa Marekani na washirika wake barani Ulaya, wataalamu na wanasayansi vijana wa Iran wamepata mafanikio makubwa katika sekta ya nyuklia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iran Press, Mohammed Eslami, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran ameyasema hayo Jumatatu na kuongeza kuwa: “Ukhabithi na fitna ambazo wanafiki (MKO) walianza wakati wa kuibuka sekta ya nyuklia ni kwa sababu walitaka kutia dosari shughuli halali za nyuklia za Iran zenye malengo ya amani.”

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki aidha amebaini kuwa: “Wafaransa wameitendea Iran dhulma kubwa zaidi katika historia ya kadhia ya nyuklia.”  Amefafanua kwa kusema: “Walichukua dola bilioni moja za fedha za Iran ili kuwekeza katika mzunguko wa nishati ya nyuklia, lakini walisababisha uvurugaji mkubwa zaidi katika mazungumzo ya nyuklia.”

Kituo cha Nyuklia cha Bushehr kusini mwa Iran

Islami  ameongeza kuwa: Mfumo wa mionzi ya Gamma ni kwa ajili ya chakula na mazao ya kilimo ambapo wakati mfumo huu unatumiwa, huondoa uchafuzi wa mazingira na huongeza muda wa kuweza kutumiwa bidhaa kwa miezi kadhaa.

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran pia amesema: “Nishati ya nyuklia ina taathira kubwa katika maendeleo ya sayansi nyingine kutokana na upeo wake mpana, na athari zake na maendeleo yake ni ya ajabu.”