Televisheni ya CNN ya Marekani yakiri uwezo mkubwa wa droni za Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i96830-televisheni_ya_cnn_ya_marekani_yakiri_uwezo_mkubwa_wa_droni_za_iran
Kanali ya televisheni ya CNN ya Marekani imelazimika kukiri uwezo mkubwa wa mfumo wa droni na ndege zisizo na rubani za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Apr 30, 2023 03:17 UTC
  • Televisheni ya CNN ya Marekani yakiri uwezo mkubwa wa droni za Iran

Kanali ya televisheni ya CNN ya Marekani imelazimika kukiri uwezo mkubwa wa mfumo wa droni na ndege zisizo na rubani za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Maendeleo makubwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika upande wa droni na ndege zisizo na rubani yamekuwepo kwa makumi ya miaka kiasi kwamba ndege hizo za Iran zimeonesha uwezo wake mkubwa katika mapigano yaliyotokea kwenye eneo hili tena katika nyuga zote za uchunguzi wa kijasusi, kutunga shabaha na kuendesha operesheni katika medani za vita.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi sasa ni miongoni mwa nchi chache duniani zenye uwezo mkubwa wa kubuni, kutengeneza na kuendeleza aina tofauti za ndege zisizo na rubani.

Televisheni ya CNN ya Marekani imekiri kuwa, mifumo ya ndege zisizo na rubani ya Iran ina uwezo mkubwa wa kupiga shabaha, kuendesha operesheni na kukabiliana na udukuzi wa maadui wanaojaribu kuvuruga mawasiliano ya ndege kama hizo.

Droni, yaani ndege zinazoruka bila ya kuwa na rubani ni miongoni mwa silaha za kisasa kabisa ambazo ni muhimu sana katika nyuga zote za kijeshi na zisizo za kijeshi.