-
Grossi: Wakaguzi wa wakala wa IAEA wamerejea Iran
Nov 19, 2025 08:35Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amesema katika kikao cha robo mwaka cha Bodi ya Magavana ya wakala huo kwamba: "Wakaguzi wa IAEA wamerejea Iran na wamefanya ukaguzi katika vituo ambavyo havikuathiriwa na mashambulizi ya Juni, lakini ushirikishwaji zaidi unahitajika ili kurejesha ukaguzi kamili."
-
Rais Pezeshkian: Iran inalenga kuimarisha uhusiano na Oman
Nov 19, 2025 03:29Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesifu uhusiano imara kati ya Iran na Oman, na kueleza kuwa Tehran ina imani kwamba uhusiano wa pande mbili utaendelea kukua kwa "nguvu na uthabiti.
-
Rais Samia: Ghasia za uchaguzi zinaweza kuathiri upatikanaji wa fedha
Nov 19, 2025 03:28Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania jana alisema kuwa ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa Oktoba 29 zinaweza kuathiri upatikanaji wa ufadhili wa kimataifa kwa nchi hiyo.
-
Watu 15 wauawa katika hujuma ya anga ya Israel katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina huko Lebanon
Nov 19, 2025 03:28Utawala wa Israel umefanya mashambulizi ya anga na kuuwa watu wasiopungua 15 kwenye kambi kubwa zaidi ya wakimbizi wa Kipalestina kusini mwa Lebanon.
-
WFP yatahadharisha kuhusu ongezeko la njaa duniani
Nov 19, 2025 03:27Mpango wa Chakula Duniani (WFP) umeeleza kuwa kupunguzwa kwa misaada ya nchi wafadhili kutazidisha mgogoro wa njaa unaozidi kuongezeka kote ulimwenguni, na kuonya kwamba zaidi ya watu milioni 300 watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula mwaka ujao.
-
'Siku ya fedheha’: Afisa wa zamani wa haki za binadamu wa UN akosoa azimio la UNSC kuhusu Gaza
Nov 19, 2025 03:26Afisa wa ngazi ya juu wa zamani wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amelaani hatua ya Baraza la Usalama la umoja huo ya kupitishaa azimio linalounga mkono mpango wa Marekani wa kuanzisha kikosi cha kimataifa cha kurejesha utulivu katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, akiitaja kura hiyo kuwa ni "siku ya fedheha" kwa chombo hicho cha dunia.
-
Bin Salman: Tunajaribu kupatanisha baina ya Iran na Marekani
Nov 18, 2025 23:19Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia ambaye kimsingi ndiye kiongozi nambari moja wa nchi hiyo amesema: "Tutafanya kila tunavyoweza kuhakikisha kunafikiwa makubaliano kati ya Iran na Marekani; (ninaamini kwamba) Tehran pia iko tayari kusaini makubaliano hayo."
-
Iran yapendekeza mfumo wa malipo wa kidijitali katika Jumuiya ya Shanghai
Nov 18, 2025 22:54Mohammad Reza Aref Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran amependekeza kuanzisha mfumo wa pamoja wa malipo ya kidijitali ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi 10 wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO).
-
Onyo la Afrika Kusini kuhusu njama ya kuwahamisha Wapalestina kwa nguvu
Nov 18, 2025 22:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Ronald Lamola, amesema kuwasili Johannesburg wiki iliyopita kwa ndege iliyobeba wakimbizi wa Kipalestina ni “operesheni iliyopangwa waziwazi” ya kuwahamisha Wapalestina.
-
Mkuu wa jeshi la Nigeria aagiza kutafutwa usiku na mchana mabinti wa shule waliotekwa nyara
Nov 18, 2025 22:53Jenerali wa ngazi ya juu wa jeshi la Nigeria ameviagiza vikosi vya jeshi hilo kuendesha msako wa "usiku na mchana" ili kuwanusuru mabinti 25 wa shule waliotekwa nyara kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.