-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani: EU siyo inayoainisha sheria za kimataifa
Nov 14, 2025 04:07Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio amesema, nchi yake haitakubali mahubiri yanayotolewa na Umoja wa Ulaya EU kuhusu jinsi inavyoendesha shughuli zake za usalama wa taifa na akapuuza ukosoaji wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kwa mashambulizi ya kijeshi yanayofanywa na Marekani kuzilenga boti zinazopita eneo la Carribean.
-
Iran yapinga na kuyatoa maanani madai ya kundi la G7 dhidi yake
Nov 13, 2025 23:52Esmail Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, madai yaliyomo kwenye taarifa iliyotolewa mwishoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zinazounda G7 uliofanyika nchini Canada kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayana msingi wala nadhari na hayakubaliki.
-
Maafa ya vita vya kinyama vya Israel yamepelekea Wapalestina 6,000 wa Ghaza kukatwa viungo
Nov 13, 2025 23:07Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza imetoa ripoti inayoonyesha kuwa, Wapalestina 6,000 wamekatwa viungo katika eneo hilo tangu utawala wa kizayuni wa Israael ulipoanzisha vita vya kinyama Oktoba 2023 ambavyo vimeendelea kwa muda wa miaka miwili.
-
UN: Raia 114 wameuawa Lebanon katika ukiukaji wa usitishaji vita uliofanywa na Israel
Nov 13, 2025 23:07Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema ukiukaji wa usitishaji vita uliofanywa Israel uliotokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya utawala huo wa kizayuni na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu nchini Lebanon ya Hizbullah mnamo Novemba 2024 umesababisha vifo vya raia 114 wa nchi hiyo.
-
Russia: Tumejiweka tayari kikamilifu kukabiliana na vitisho vya kijeshi vya Magharibi
Nov 13, 2025 23:03Msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov amesema, Moscow ina uelewa kamili kwamba nchi za Magharibi zinajizatiti upya kijeshi kwa makabiliano zinayoweza kuanzisha dhidi Russia, na kwamba Moscow nayo imeshajiweka tayari kikamilifu kwa sinario kama hiyo.
-
Umoja wa Mataifa watahadharisha kuhusu hatari ya njaa katika nchi 16
Nov 13, 2025 22:55Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) zimeonya kuhusu mgogoro mkubwa wa ukosefu wa usalama wa chakula unaozidi kuwa mbaya katika nchi 16, na kuweka hatarini maisha ya mamilioni ya watu, hasa katika maeneo yenye migogoro na majanga ya hali ya hewa.
-
Mgogoro wa kisaikolojia miongoni mwa wanajeshi wa Israel; Wizara ya Vita ya Israel: Kujiua wanajeshi ni kielelezo cha kushindwa
Nov 13, 2025 22:54Gazeti la Uingereza The Independent, limeashiria ongezeko la kiwango cha kila mwaka cha kujiua katika jeshi la Israel baada ya vita vya Gaza, na kuandika kuwa: "Zaidi ya wanajeshi 11,000 wa Israel wamekumbwa na aina mbalimbali za matatizo ya kisaikolojia baada ya vita hivyo, na takwimu kuhusu wanajeshi wanaojiua baada ya kuondoka jeshini hazijachapishwa."
-
Bunge la Tanzania lamthibitisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo
Nov 13, 2025 10:20Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Alhamisi limemthibitisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo baada ya kupata kura 369 kati ya kura 371 zilizopigwa na wabunge. Baada ya uthibitisho huo, Dkt. Nchemba ataapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuanza mara moja majukumu yake.
-
Mudavadi: Zaidi ya Wakenya 200 wanapigana pamoja na Russia katika vita vya Ukraine
Nov 13, 2025 10:19Serikali ya Kenya imesema kwamba zaidi ya raia wake 200 wanapigana katika safu ya jeshi la Russia katika vita vyake dhidi ya Ukraine, ikionya kwamba mitandao ya kuajiri wapiganaji bado inaendelea kufanya kazi na inawalenga Wakenya kwa kutoa kazi zenye kipato kikubwa.
-
Ni ipi nafasi ya pande za kigeni katika mgogoro wa Sudan?
Nov 13, 2025 09:25Vita nchini Sudan vimechukua sura mpya kufuatia kuendelea uingiliaji kati wa nchi ajinabi nchini humo na kudhibitiwa mji wa Al Fasher na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).