Mar 28, 2024 06:53 UTC
  • Marekani imeshindwa kukabiliana na jeshi la Yemen katika Bahari Nyekundu

Viongozi wa Marekani wamekiri kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na jeshi la Yemen katika Bahari ya Shamu. Hii ni kufuatia kuendelea makablinao ya Magharibi chini ya uongozi wa Marekani dhidi ya jeshi la Yemen katika Bahari Nyekundu.

Katika hali ambayo Marekani inatekeleza oparesheni kwa jina la "oparesheni ya kudhamini usalama" katika Bahari Nyekundu kwa zaidi ya miezi mitatu sasa, lakini Admeri Mark Meig kamanda wa jeshi la Marekani wa meli ya USS Eisenhower inayobeba ndege za kivita amekiri kuwa nchi hiyo na washirika wake wanapasa kufanya kazi kubwa ili kulishinda jeshi la Yemen. 

Amesema, hatua kadhaa ziliochukuliwa hadi sasa hazitoa ulinzi wa kutosha kwa makampuni ya usafirishaji wa baharini. 

Wakati huo huo Ralf Haben Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hapag Lloyd yenye makao yake mjini Hamburg Ujerumani pia ameeleza kuwa inahofiwa kwamba usafiri wa baharini katika Bahari Nyekundu utaendelea kuvurugika hadi mwaka 2025. 

Haben amesisitiza kuwa jeshi la Yemen katika miezi ijayo litakuwa na uwezo wa kuzishambulia meli kwa kasi hiyo hiyo ya hivi sasa.

Jeshi la Yemen lilianza kuzishambulia meli zenye mfungamano na utawala wa Kizayuni zinazoelekea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) sambamba na kuanza mashambulizi ya kikatili ya utawala huo dhidi ya wakazi wa Kipalestina huko Ukanda wa Gaza. 

Mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Gaza