Jan 29, 2023 08:01 UTC
  • Wanamuqawama watekeleza oparesheni 57 dhidi ya Wazayuni katika saa 24 zilizopita

Chombo kimoja cha Kizayuni kimetangaza kuwa makundi ya muqawama ya Palestina yametekeleza oparesheni 57 dhidi ya Israel katika saa 24 zilizopita.

Kabla ya hapo Wapalestina walikuwa wakipambana na Wazayuni huko kusini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na katika Ukanda wa  Ghaza, lakini  hivi sasa eneo la Ukingo wa Magharibi huko mashariki mwa Palestina limeguzwa na Wazayuni maghasibu kama ngome yao baada ya vijana wa Kipalestina kuamua kubeba silaha kupambana na wanajeshi wa Israel na hivyo kuwanyima usingizi Wazayuni hao.  

Televisheni ya 14 ya utawala wa Kizayuni imekiri kuwa tangu juzi Jumamosi hadi sasa makundi ya wanamuqawama wa Palestina yametekeleza oparesheni 57 dhidi ya Wazayuni maghasibi katika Ukingo wa Magharibi na quds inayokaliwa kwa mabavu. 

Wakati huo huo vyombo vya habari vya Kizayuni jana usiku vilidai kuwa kijana mmoja wa Kipalestina alijaribu kuwafyatulia risasi walowezi wa Kizayuni katika kitongoji cha Kedumim ambapo Mpalestina huyo aliuliwa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Kizayuni.  

Duru za habari za utawala wa Kizayuni jana  zilitangaza kuhusu ufyatuaji risasi uliojiri katika kitongoji cha Silwan katika mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu ambapo Wazayuni wawili walijeruhiwa katika tukio hilo. Hiyo ilikuwa ni oparesheni ya pili dhidi ya Wazayuni kutekelezwa na wanamuqawama wa Palestina katikamuda wa chini ya masaa 24 huko Quds inayokaliwa kwa mabavu. 

Mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu juzi Ijumaa pia ulishuhudia oparesheni ya kujitolea kufa shahidi iliyofanywa na Khairi Alqam, aliyekuwa na miaka 21 akijibu jinai za karibuni za Wazayuni  katika mji wa Jenin. Oparesheni hiyo dhidi ya Wazayuni iliwaangamiza na kuwajeruhi Wazayuni 12; ambapo baadhi ya duru zinasema kuwa Wazayuni 10 wameuliwa kwenye oparesheni hiyo. 

Wazayuni waangamizwa katika oparesheni ya kijana Mpalestina