Shauku ya uchaguzi nchini Iran/ Tweeti za watumiaji mitandao wa Iran kuhusu uchaguzi wa rais
(last modified 2024-07-17T11:46:17+00:00 )
Jul 17, 2024 11:46 UTC
  • Shauku ya uchaguzi nchini Iran/ Tweeti za watumiaji mitandao wa Iran kuhusu uchaguzi wa rais

Pars Today- Wakati huo huo siku ya uchaguzi wa rais nchini Iran inakaribia, watumiaji wa Iran wa mtandao wa kijamii wa X, kama watu wengine wa Iran, wanafuatilia uchaguzi huu kwa msisimuko na shauku maalum.

Tarehe 19 Mei, Seyed Ebrahim Raisi, rais wa nane wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alihusika katika ajali ya ndege alipokuwa akirejea kutoka kwenye sherehe za ufunguzi wa bwawa kaskazini magharibi mwa Iran, ambapo aliuawa shahidi pamoja na Hossein Amirabdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje, na viongozi wengine.

Kwa mujibu wa Ibara ya 131 ya Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kufuatia tukio la rais kufa, kujiuzulu, kuugua kwa zaidi ya miezi miwili, kuachishwa kazi au sababu nyinginezo kama hizo, Baraza la Muda la Rais linawajibika kupanga uchaguzi wa rais mpya ndani ya siku hamsini.

Kwa kuzingatia hili, uchaguzi wa awamu ya kumi na nne ya urais ulifanyika tarehe 28 Juni, 2024.

Kuhusiana na hili, tumekuchagulieni tweets 10 za watumiaji wa mitandao ya kijamii ambazo unazisoma kama ifuatavyo:

Ukosoaji wa siasa za kundumakuwili za Marekani kuhusu uchaguzi wa Iran

Mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X kwa jina "Absolute Zero" katika tweet amekosoa siasa za kundumakuwili za Marekani kuhusu kususiwa uchaguzi wa Iran.

Ameandika: Kwao wao wanahimiza kushiriki kwenye uchaguzi na kwetu sisi kususiwa uchaguzi!

Ukosoaji wa mtumiaji wa X dhidi ya siasa za kindumakuwili za Marekani kuhusu uchaguzi wa Iran

Uchaguzi ni fursa ya kuongeza ufahamu na mwamko

Massoud Barati, mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X, ameutaja uchaguzi wa rais wa Iran kama fursa ya kuinua kiwango cha ufahamu na mwamko wa watu.

Ameandika: Uchaguzi ni fursa ya kuinua kiwango cha ufahamu na mwamko wa watu. Fursa hii hupatikana kutokana na juhudi za kutafuta na kumtambua mtu (mgombea) anayefaa zaidi. Kila fikra na siasa zinazopelekea kupotea fursa hii ni kinyume na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Tweet ya Barati kuhusu uchaguzi, fursa ya kuongeza ufahamu na mwamko

 

Uamuzi wa leo = mafanikio ya kesho

"Mohammed Mehdi", mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X, katika chapisho, alizingatia uamuzi wa watu wa Iran wa kumchagua rais leo kama msingi wa mafanikio ya Iran kesho.

Ameandika: Mafanikio ya kesho yanategemea uamuzi wa leo, mimi nitapiga kura, wewe je?

Tweet ya Mohammed Mehdi kuhusu mafanikio ya kesho yanategemea uamuzi wa leo

Kutoiamini Magharibi

Saeed Pouya, mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X, ametangaza sharti la kumchagua mgombea wake katika uachaguzi ujao kuwa ni msimamo alionao kuhusu kutoziamini nchi za Magharibi.

Ameandika: Katika uchaguzi wa rais, mwaminini mtu ambaye haamini tabasamu la nchi za Magharibi.

Tweet ya Saeed Pouya kuhusu kutoziamini nchi za Magharibi

 

Uchaguzi ni jambo la mafanikio

Razieh Bakhtiari, mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X, ameutaja uchaguzi katika tweet kuwa jambo lenye mafanikio.

Ameandika:

Uchaguzi ulio mbele yetu ni jambo lenye mafanikio. Iwapo, Mungu akipenda, utafanyika kwa ushiriki mkubwa wa watu, hayo yatakuwa mafanikio makubwa kwa taifa la Iran. Baada ya tukio hili chungu, kama watu watakusanyika na kumchagua rais anayefuata kwa kura nyingi, jambo hili litakuwa na taathira kubwa ulimwenguni.

Tweet ya Razieh Bakhtiari kuhusu mafanikio ya uchaguzi

 

Sisitizo la kuheshimu maadili ya uchaguzi

Hossein Harandi, mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X, amesisitiza umuhimu wa kuzingatiwa maadili ya uchaguzi na wagombea wa kiti cha rais na wafuasi wao.

Harandi ameandika:

Katika uchaguzi huu acheni mradi wa kulipiza kisasi na teteeni haki tu. Mara hii mambo ni tofauti, hali ya dunia ni ngumu sana, tunazungumzia mustakabali wa Iran! Ni lazima tuwajibike mbele ya Mwenyezi Mungu na mashahidi kwa maneno tunayoandika.

Tweet ya Hossein Harandi kuhusu kuzingatia maadili ya uchaguzi

 

Katika muktadha huu, Amir Chizari, mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X ameandika:

Kuwa makini kabla ya kushindwa/kushinda uchaguzi! Usishindwe duniani na Akhera.

Tweet ya Amir Chizari kuhusu kuzingatia maadili ya uchaguzi

 

Mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X kwa jina H_Eghbalian pia ameandika kuhusu suala hili:

Tukumbuke kuwa kuharibu jina na kumvunjia heshima mgombea mpinzani ni kumharibia jina kwa njia isiyo ya moja kwa moja, mgombea tunayemuunga mkono na jambo hilo litakuwa na taathira mbaya kwake. Msijiingize goli wenyewe, jamani.

Tweet ya mtumiaji wa X kuhusu kuchunga maadili ya uchaguzi

 

Kumchagua mtu anayefaa zaidi

Meysham Vaesi mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X anaona ni muhimu kumpigia kura mtu mstahiki na anayefaa zaidi katika uchaguzi wa rais wa Iran.

Vaesi anaandika:

Mtu anapaswa kumchagua mtu ambaye amekuwa kwenye njia ya kutoa huduma.

Tweet ya Meytham Vaesi kuhusu kuchaguliwa mtu anayefaa zaidi

 

Kukubali mfumo wa Walii Mtawala

Mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X anayeitwa  Neda.darabi ameandika kwenye tweet yake, akiashiria utiifu wa Rais Shahidi wa Iran, Sayyid Ebrahim Raisi, kwa mfumo wa Walii Mtawala na kusema kuwa suala hilo ni sharti muhimu la kuchaguliwa mtu anayetaka kuwa rais wa nchi.

Ameandika:

Katika uchaguzi ujao, mchagueni yeyote anayezingatia suala hili, mtu kama Sayyid wetu Shahidi...

Tweet ya mtumiaji wa X kuhusu umuhimu wa rais wa Irani kukubali mfumo wa Walii Mtawala

 

Tags