Aug 06, 2024 11:13 UTC
  • NATO ni wenzo wa uhalifu wa Wamagharibi/angalia tweets za watumiaji wa X

Pars Today- Uhalifu wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO) haufichiki kwa mtu yeyote. Ni kwa sababu hiyo ndio maana Alfred Dozias, mtaalamu wa zamani wa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, analichukulia shirika hilo kuwa ni tishio kubwa zaidi kwa usalama wa binadamu duniani.

Katika ripoti hii kutoka Pars Today, tumeangalia tweet muhimu za watumiaji wa mtandao wa kijamii wa "X" kuhusu tabia na uingiliaji wa NATO wa mambo ya ndani ya mataifa mengine duniani.

Uhalifu wa NATO

Mmoja wa watumiaji wa mtandao wa X aliyejitambulisha kwa jina la "lookingnLearning" anataja baadhi ya uhalifu wa "NATO" na kuandika:

"Hali imebadilika, lakini maadili ya magenge yenye silaha ya NATO na shimo la bwana wao hayajabadilika, kutoka uhalifu wao huko Yugoslavia hadi kuunda mashine za kusaga nyama nchini Ukraine; kutoka magendo ya mihadarati hawi kufanya magendo ya viungo vya wanadamu."

Tweet ya mtumiaji wa mtandao wa X kuhusu uhalifu wa NATO

 

 

 

Namna "NATO" ilivyo kibaraka

 

"Mahdi Atezadi" mmoja wa wanaharakati wa masuala ya kisiasa naye pia anaihesabu NATO kuwa ni kibaraka na chombo cha uhalifu kinachotumiwa vibaya na Waingereza na Wademokrati wa Marekani. Anasema:

 

"Mudwa wote bajeti ze chombo hiki zinatolewa kwa ajili ya kuisambaratisha Yugoslavia na kufanya mapinduzi Romania na mapinduzi ya mahameli huko Ukraine na ya Chama cha Mshikamano cha Poland sambamba na mauaji katika nchi Misri na Libya na sasa huko Ghaza na Ukraine. NATO ni chombo cha uhalifu wa Uingereza na Wademokrat. Lakini kuna siku uhalifu huu utaisha."

Tweet ya Mahdi Atezadi kuhusu namna NATO ilivyo kibaraka

 

 

Vitisho vya kifedhuli vya NATO dhidi ya Russia

 

Milad Rezaei, mtumiaji mwingine wa mtandao wa kijamii wa X, aliyataja mashambulizi ya kigaidi dhidi ya miji ya Makhachkala na Darband ya Jamhuri ya Dagestan kuwa ni ushahidi wa jinsi NATO ilivyotumia matukio hayo kutoa vitisho vya kifedhuli dhidi ya Russia. Ameandika:

 

"Jana kulifanyika shambulio la kigaidi katika maeneo mawili huko Dagestan, na shambulio hilo lilionesha namna ubeberu wa Magharibi yaani chombo chake cha kijeshi, NATO, kilivyoamua kutoa vitisho na kuishinikiza Russia kwa kutumia vitendo vya kigaidi."

 

Tweet ya Milad Rezaei kuhusu vitisho vya kifedhuli vya NATO dhidi ya Russia.

 

 

NATO inavyochochea moto wa vita

 

"Mohamadreza Shokouhifard" mwanaharakati mwingine wa mtandao wa kijamii wa X ametuma ujumbe kwenye mtandao huo akizungumzia uchochezi wa Marekani na NATO akisema:

 

"Jeshi la Ukraine limeshambulia ufukwe wa burudani nchini Russia kwa kutumia makombora ambayo lilipokea hivi majuzi kutoka kwa Marekani. Kufikia sasa, takriban watu 10 wameuawa, ambapo 5 ni watoto. Ikiwa huu si mfano wa ugaidi wa serikali inayofanya mashambulizi kwa niaba ya Marekani, basi ni nini? Biden na wenzake katika NATO wanaonekana wameamua hasa kuwasha moto wa Vita vya Tatu (vya Dunia).

 

Twitter ya "Mohamadreza Shokouhifard" ugaidi wa NATO

 

 

Mtumiaji anayejiita "MdTaghi" pia aliwaita wanachama wa NATO kuwa ni magaidi na kuandika:

 

"Inavyoonekana, Bwana Putin hatimaye amegundua uhusiano wa karibu mno uliopo baina ya magaidi wa NATO, Israel na Daesh yaani ISIS. Natumai ushauri wa dhati wa mpendwa Hajj Qassem Soleimani, ambaye alionesha jinsi ilivyotekelezwa diplomasia ya kuwa na uhusiano mzuri na majirani na marafiki wa Russia."

 

Tweet ya mtumiaji wa X kuhusu ugaidi wa NATO

 

 

"Mahmoud Rezaei," mwanaharakati mwingine wa mtandao wa X, anaiona NATO na washirika wake katika hali dhaifu na anasisitiza kwa kukandika:

 

"Israel, Magharibi na NATO, hawana uthubutu wa kuingia vitani wakati vita vitakavyopotea. Hivyo kushambulia maeneo ya raia ndilo jambo pekee watakalofanya. Lakini ni wazi kwamba kulivunja nguvu jeshi la anga la NATO kunamaanisha kushindwa kwao, na kushindwa kwa NATO nchini Ukraine ni pigo kubwa kwao."

 

Tweet inayoonesha jinsi Israel, Magharibi, NATO na vibaraka wao wasivyo na uwezo wa kuingia kwenye vita vya kweli

 

 

Tags