Kuhusu hatua ya Saudia ya kuwazuia Wairani kwenda Hija mwaka huu
Serikali ya Saudi Arabia imeweka vizingiti vingi vya kuwazuia wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwenda Hija mwaka huu.
Mwandishi wa Shirika la Habari la Kimataifa la Qur'ani Tukufu IQNA, amemnukuu Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran, Dk Ali Ahmad Jannati akisema siku ya Jumapili kuwa, Saudia imeweka vizingiti vingi na kufanya njama mbalimbali haribifu ili kuwazuia Waislamu wa Iran kwenda Hija mwaka huu.
Ameongeza kuwa, maafisa wa Saudia wamekuwa na muamala mbovu kwa wajumbe wa Iran waliokwenda nchini humo mara mbili kwa ajili ya mazungumzo kuhusu Hija.
Tumezungumza na Ustadh Abdul Razaq Rashid, msomi na mchambuzi wa masuala ya ulimwengu wa Kiislamu ambaye hivi sasa yuko mjini Qum hapa Iran. Ingia katika picha hapo juu kusikiliza mahojiano yenyewe.